
Ufunuo wa Yohana 3
²⁰ Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.
Haya ni maneno ya Yesu Kristo kwa kanisa la mwisho yaani Laodikia. Yapo makanisa saba au nyakati saba za kanisa kama tulitangulia kuona ambazo Yesu Kristo ametuma ujumbe tofauti tofauti kuonya juu mwenendo wa kila kanisa. Nyakati ya mwisho ya kanisa ni hii ambayo Kristo hayupo ndani ya kanisa, badala yake anabisba apate kuingia.
MLANGO UPI ANABISHA?
Mlango anaobisha ni wa kanisa hili la Laodikia, sio kama walokole wasemavyo kuwa anabisha kwenye moyo wa mtu aokoke. Wao hutafsiri hivi kwa sababu injili yao ni maziwa (waebrania 5:12-14). Mlango anaobisha ni mlango wa kanisa. Na kimsingi ni kanisa la wapentekoste, maana hawa ndio Laodikia.
Lakini Laodikia au wapentekoste si kanisa moja bali madhehebu mengi, na si madhehebu yote yaliyopo leo ni ya Laodikia, bali yapo na yale ambayo yamekiwepo kabla ya Laodikia, yaani kabla ya mwaka 1906. Nayo pia ni Laodikia kwa sababu yameifikilia nyakati ya Laodikia.
Hivyo Laodikia ni moja, lakini ina madhehebu mengi. Na kwa maana hiyo mlango anaobisha si mmoja bali ni milango mingi. Milango hiyo ndio madhehebu yaliyopo leo. Anabisha akiwa nje apate kuingia ndani.
KWA NINI YUPO NJE?
Kila kanisa au dhehebu linajua kuwa Kristo yumo ndani yao. Si ndani ya kanisa tu bali ndani ya miili yao kulingana na neno la huyo huyo Kristo.
20 Siku ile ninyi mtatambua ya kuwa mimi ni ndani ya Baba yangu, nanyi ndani yangu, nami ndani yenu.
Yohana 14
Lakini katika nyakati za mwisho kwa nini hayupo ndani, na badala yake anagonga mlango akiwa nje? Dhambi ya uvuguvugu imemtoa nje bila kanisa kutambua.
Ufunuo wa Yohana 3
¹⁴ Na kwa malaika wa kanisa lililoko Laodikia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye Amina, Shahidi aliye mwaminifu na wa kweli, mwanzo wa kuumba kwa Mungu.
¹⁵ Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto.
¹⁶ Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu.
Hilli ndio kosa ndani ya kanisa, Laodikia amemezwa na uvuguvugu ambao ni chukizo kwa Bwana. Lakini kanisa hili vuguvugu yaani madhehebu wanaendelea kukariri maneno yake kuwa yupo ndani yetu.
ATAINGIA NDANI YA KANISA TENA?
Jibu la swali hili linangoja hata sasa, maana amesimama mlangani hata sasa. Kristo ni Neno la Mungu, nalo lipo mlangoni hata sasa.
Kama ilivyokuwa kwa wayahudi, walimngoja masihi wakidhani akitokea atakuwa na sifa zile zile walizofundishwa kwenye theolojia, hekima za wanadamu. Wakangoja mwanadamu kisha likaja neno la Mungu juu yao wasimtambue waliemngoja.
Kristo kuingia ndani ya kanisa ni kanisa kutubu kulingana na injili yake iliyo moto ili kuondoa uvuguvugu. Hivyo kusimama mlangoni ni neno la Kristo kwa madhehebu, kwa watu walio ndani ya kanisa. Mara ya kwanza hakuja isipokuwa kwa kondoo waliopotea. Hakuja isipokuwa kwa ajili ya hao waliokuwa na neno lake lakini wakawa vuguvugu.
KWA NINI MLANGO WA MADHEHEBU UMEFUNGWA?
Ufunuo wa Yohana 3
²⁰ Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, NA KUUFUNGUA MLANGO, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.
Mlango unaozungumziwa hapo sio hii ya mbao au chuma. Mlango huu nii ile theolojia ya lile dhehebu. Kila theolojia ambayo ndiyo mafundisho ya lile dhehebu imesimama kama Yesu Kristo kwa lile dhehebu, ni kamilifu machoni pa lile dhehebu hata kama si kamilifu mbele za Mungu.
Hivyo kila theolojia inachukuliwa kama imani ya lile dhehebu pamoja na makosa yake. Maana yake kila theolojia imefunga mlango wa kuongezewa kwa kujiona kamilifu isipokuwa nyongeza iwe kutoka kwa walimu wa theolojia hiyo ambao kimsingi wao pia hawawezi kuongeza au kupunguza. Na wakifanya hivyo hutengwa na lile dhehebu.
Hakuna theolojia iliyo sahihi, kwa sababu theolojia zimetokana na ufunuo wa damu na nyama na ufunuo wa watoto wadogo. Kila theolojia inatabia na roho wake yenyewe tofauti na Roho wa Mungu, kwamba kila tafsiri waliyonayo ni sahihi kulingana na tabia ya ile theolojia au roho ya ile theolojia yao. Ndipo kwa nini Roho wa Mungu anakuwa hana nafasi ndani ya kanisa kwa sababu kanisa haliendi kwa Roho wa Mungu.
Roho hizi za madhehebu zimefunga mlango ili roho nyingine isiingie pamoja na Roho wa Mungu. Hivyo kila dhehebu ni kamilifu machoni pake lenyewe na kwa sababu halitazamii kutubu kwa kujiona halina makosa machoni pake. Limefunga mlango kusikia neno lolote isipokuwa hilo walilo nalo na roho yao wenyewe.
Hivyo Kristo anaposema nasimama mlangoni, nabisha, MAANA YAKE ANASIMAMA KINYUME NA KILA THEOLOJIA. Mtu akiisikia sauti yake kwa maana ya kuielewa injili anayohubiri na kujua makosa na kutubu huyo ndiye Kristo ataingia ndani yake. Kwamba ni mtu binafsi au dhehebu zima.
Maana yeye hatalichanganya neno lake na uongo, hatalichanga neno lake na theolojia fulani kwa maana imeandikwa;
22 Wala hakuna mtu atiaye divai mpya katika viriba vikuukuu; ikiwa atia, ile divai mpya itavipasua viriba vile, divai ikamwagika, vile viriba vikaharibika. Bali hutia divai mpya katika viriba vipya.
Marko 2
Divai mpya ndio neno la Mungu na viriba vikuukuu ndio madhehebu. Kwa sababu hiyo haiwezekani kulichanganya neno la Mungu katika theolojia za madhehebu. Lakini kila dhehebu linamsubiri Yesu arudi, tena wanamsubiri kwa hamu. Na kila dhehebu kama ilivyokuwa kwa madhehebu ya kiyahudi kabla ya Kristo, lilimsubiri kulingana na theolojia yao.
Tazama, yupo mlangoni pako leo, ambaye hata ukimwona huwezi kusadiki habari zake kwa sababu anapingana na theolojia yako na kukutaka utubu. ISIKILIZENI SAUTI YA BWANA.
Mawasiliano
+255 755 251 999