top of page

Kunena kwa lugha ni kuomba kwa msaada wa Mungu, kwamba unakuwa unanena maneno ambayo hayatokani na fahamu 

wala akili zako. Hutamka maneno lakini hayatoki kwa huyu aombaye anaomba bali anasaidiwa na Mungu.


26 Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.

Warumi 8:26


Haya ni maneno ya Paulo akizungumzia jambo hilo hilo kwamba, kwa kuwa hatuwezi kuomba itupasavyo, ndipo  Roho mtakatifu hutusaidia kuomba kwa kutupa maneno yaliyo nje ya fahamu na akili zetu. 


Mtu anaponena kwa lugha anakuwa ameshukiwa na nguvu kutoka juu ili kupewa msaada wa kuomba katika haja aiombayo. Huyo mtu anayenena kwa lugha huingia ndani ya Roho mtakatifu na Yeye ndani ya huyo mtu. 


Roho mtakatifu anampa msaada wa kunena ipasavyo katika kuugua kwa namna ambayo mwanadamu kwa namna ya kawaida hawezi kufikia. Hivyo kunena kwa lugha pasipo roho mtakarifu haiwezekani.


KUNENA KWA LUGHA KWA WASIO HAKI


Wasio haki ni watu waliokuwa katika njia ya kweli, wakageuka, mmoja kulia na mwingine kushoto kama Adamu. Wakamhuzunisha Roho mtakatifu na kumzimisha ndani yao pasipo kujua kwao. Kwa kuwa hawajui kuwa wamemzimisha Roho mtakatifu ndani yao, wala kuyajua makosa yao, huendelea mbele kana kwamba yumo ndani yao.


Na kwa sababu kazi za Roho mtakatifu hazitendeki pasipo yeye, huendelea kutoweka ndani ya kanisa hata kukoma kabisa. Lakini watu wale au kanisa kwa kuwa wana hekima machoni pao, hawawezi kujiuliza tumekosea nini? Mbona amepungua na amezidi kufanya hivyo hata hayuko pamoja nasi tena?


Badala yake huendelea katika njia yao, na ili kuifanya hekima yao ya kibinadamu ionekane ndio! Huweka maneno yao badala ya Roho mtakatifu kwa mfano wa yale ya Roho mtakatifu. Kama Paulo alivyofanya wakati akitoa mfano kanisani.


19 lakini katika kanisa napenda kunena maneno matano kwa akili zangu, nipate kuwafundisha wengine, zaidi ya kunena maneno kumi elfu kwa lugha.

1 Wakorintho 14:19


Paulo wakati anafundisha kunena kwa lugha alitumia maneno kadhaa kwa mfano wa yale anayoyanena wakati ameshukiwa na Roho mtakatifu. Hawezi kutolea mfano kwa maneno halisi ya roho mtakatifu kwa sababu hayatoki kwake bali kwa Roho mtakatifu.


Hivyo akaamua kutumia maneno mawili matano wakati anafundisha ili kuwafanya wengine wajue kunafananaje. Maneno hayo matano aliyoyatumia mfano aliyatunga yeye mwenyewe kwenye akili zake. 


Jambo ambalo kila mtu anaweza kufanya hivyo awe ameokoka au hajaokoka. Maana ni kutamka maneno yoyote yasiyoeleweka kwa wanadamu au akaongea lugha yoyote isioelewea na watu walio karibu. Kwa kufanya hivyo unakuwa unaigiza na si kunena kwa uhalisia.


Paulo aliigiza kunena kwa lugha katika kanisa ili kuwapa elimu juu ya kunena kwa lugha pale nguvu ya Mungu iwashukiapo. Kuigiza tunakufahamu, kama watu wanavyoigiza filamu, mmoja akaigiza anapigana vita wakati kiuhalisia hajawahi kuwa katika vita, maana yake anafanya kwa ajili ya wanadamu.


Hivyo leo utaona makanisa ya kilokoke, kilutheri, na hata anglikan yaani kiujumla makanisa ya kipentekoste wakinena kwa lugha kwa akili zao, bila Roho mtakatifu kama kunena kwa lugha halisi. Wanaigiza kama alivyoigiza Paulo wakati akifundisha katika kanisa, lakini hawa wanaigiza wakijua kuwa ndivyo inavyopaswa.


Wanafanya hivi kwa ajili ya wanadamu waamini kuwa Mungu yupo pamoja nao. Na pia wao wenyewe kuendelea kujitia moyo na kuendelea mbele katika njia zao na mawazo yao yaliyo nje ya neno la Mungu.


Tazama hili neno la Mungu kwa wapentekoste (waigizaji).


14 Na kwa malaika wa kanisa lililoko Laodikia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye Amina, Shahidi aliye mwaminifu na wa kweli, mwanzo wa kuumba kwa Mungu. 
15 Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto. 

16 Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu
17 Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi. 

Ufunuo wa Yohana 3:16-17.


Hapa ni kanisa la saba na la mwisho, ambalo ndio wapentekoste, Kristo anasema si baridi wala moto, na kwa kuwa ni Vuguvugu atalitapika litoke kwake. Moja kwa moja inaeleza kosa la kanisa na kwa nini Roho mtakatifu ameondoka ndani ya kanisa kuwa ni uvuguvugu.


Hayuko ndani bali yuko nje akigonga mlango apate kuingia tena na kuzitenda kazi kama hapo kwanza na hata zaidi. Lakini mlango umefungwa kama asemavyo mstari wa 20.


20 Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.


Ufunuo wa Yohana 3


Anabisha mlango wa kanisa ili kanisa lisikilize ayasemayo lipate kutubu kwa maana ya kutambua au kuelewa kosa lao na kuliacha yaani kumgeukia. Ndipo atapokuwa kwao kama hapo kwanza, akiwasaidia katika kunena kwa lugha na si kufanya maigizo.


Haya maigizo yanayoendelea leo sio kunena kwa lugha, ni maneno anayoyatunga mtu kwa akili zake ambayo wewe pia unaweza kuyatunga na mahali popote utakapokuwa, iwe ni chooni, kanisani, bar, kwenye gari, kwenye riadha, kwenye harusi, n.k. Kwa sababu haihitaji kuwa na Roho mtakarifu bali akili zako tu.


Wasio haki wanajiona wana roho mtakatifu kweli kweli kwa sababu wananena kwa lugha, huku ndio kuwa kipofu kama katika mstari wa 17 alivyonena.


17 Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na KIPOFU, na uchi

Mwisho wa siku wapentekoste hawahitaji kitu kingine kwa sababu wamejitajirisha, wananena kwa lugha, wana karama zote (katika namna hiyo hiyo ya kuigiza), wana mafundisho mazuri (hayo hayo yawatiayo uvuguvugu).


ISIKIKIZENI SAUTI YA BWANA!




MAWASILIANO;


(+255) 0755 251 999.

MATENDO YA SHERIA NI NINI NA KWA NINI HAYALETI HAKI?

NEEMA, NA MAUTI ILETWAYO NA NEEMA!

ANDIKO HUUA BALI ROHO HUHUISHA

WASIO HAKI HUNENAJE KWA LUGHA?

HAKUTAKUWA NA UNYAKUO JUU YA KIZAZI HIKI!

        CHANGIA KUPITIA

 

          NMB:       22510119402

          MOBILE: 255755 251 999

​​

             MASHIBE ELIAS NTINGINYA

Mawasiliano:

 

+255 755 251 999

Mbezi, Dar-es salaam

  • Facebook
  • Instagram
  • X
  • TikTok
bottom of page