top of page
24 Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama yamkini, hata walio wateule. 
25 Tazama, nimekwisha kuwaonya mbele. 
26 Basi wakiwaambia, Yuko jangwani, msitoke; yumo nyumbani, msisadiki.

Mathayo 24:24-26.


Hapa kuna kuna makundi mawili ya manabii wa uongo, kuna manabii wa uongo, kisha makristo wa uongo. Tuanza kuangalia moja baada ya jingine.


  1. MANABII WA UONGO


Kuna aina nyingi za manabii hawa wa uongo, hapa tuangalie chache;


1.Kuna manabii wa uongo wanaonena uongo kwa kukosa maarifa. Hawa ni wengi kuliko idadi yoyote ya manabii wa uongo, neno walilo nalo ni maziwa yaliyoghoshiwa pamoja na yanayotoka kwa wanadamu.


Hawa ndio walimu na wachungaji na maaskofu na mitume/manabii n.k waliopo makanisa. Hawa hutumia theolojia (mafundisho yaliyo maagizo ya wanadamu) kama kiongozi wa mafundisho yao.


6 Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; KWA KUWA WEWE UMEYAKATAA MAARIFA, MIMI NAMI NITAKUKATAA WEWE, USIWE KUHANI KWANGU MIMI; kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, mimi nami nitawasahau watoto wako.

 

Hosea 4:6


Hayo ni maneno yanayoonesha watu au kanisa kukosa maarifa kwa sababu ya walimu au wachungaji wao kukosa maarifa ya Mungu, isipokuwa hizo theolojia zao. Hata Mungu alipoleta maarifa kwa njia ya manabii kama Hosea , Isaya, Yeremia na wengine, walimu na makuhani na manabii n.k walikataa yale maarifa yao kwa sababu yalikinzana na theolojia zao.


Ndipo Mungu anawaambia kuwa atawakataa wao pia kwa sababu watu wake wanaangamia kwa kukosa maarifa na wakati maarifa ameshayaleta ila wao wakayazuia yasiwe kwa watu wake. 


Hivyo namna pekee iliyokuwa imebaki ni kuwatapika walimu hao. Ndivyo Kristo alivyofanya, akafanya makuhani wengine mbali na hao wa kwanza ili watu wake wasiendelee kuangamia katika uovu kwa kukosa maarifa. Na pia ndio watakaofanya kanisa wakati huu litapikwe (ufunuo 3:16). Lakini hawa ndio hushikilia kanisa lote, kuwatapika unatapika kanisa zima.


Maana aina hii ya manabii au watumishi ndio hao wanaofanya watu wasitubu maana ndio masikio na macho ya watu katika kila dhehebu. Hawajui neno litokalo katika kinywa cha Mungu isipokuwa kila neno linalotoka katika vinywa vya walimu hawa, yaani hizo theolojia zao.


Kinachowafanya kuwa wa uongo ni ule uongo wa theolojia walizorithi. Katika madhehebu na theolojia zao ni waaminifu na wa kweli. Na ndipo ukipinga uongo katika theolojia zao wanaona unapingana na Mungu na kukuona kuwa wewe ndie nabii wa uongo.


2.Kuna manabii wa uongo kwa sababu ya kutamani pesa na mali. Katika hawa ndio utakutana na majina mengi kama; nabii, na kuhani, mtume na nabii na majina kama ya wasanii wa dunia. Hawa jumla ya ujumbe wao ni amani; asubuhi amani, jioni amani, usiku amani. Yaani mabubiri yao yote ni amani, utabarikiwa, utafanikiwa, n.k.


1 Lakini kuliondokea manabii wa uongo katika wale watu, kama vile kwenu kutakavyokuwako waalimu wa uongo, watakaoingiza kwa werevu uzushi wa kupoteza, wakimkana hata Bwana aliyewanunua, wakijiletea uharibifu usiokawia. 
2 Na wengi watafuata ufisadi wao; na kwa hao njia ya kweli itatukanwa. 
3 Na katika kutamani watajipatia faida kwenu kwa maneno yaliyotungwa; ambao hukumu yao tangu zamani haikawii, wala uvunjifu wao hausinzii.

 

2 Petro 2:1-3


Na kisha kwa sadaka za udhalimu hujikusanyia tamaa ya mioyo yao na kusali sala ndefu kwa wale watu waliowaibia. Nao ndio watu wakuu sana kwa sababu ya utajiri wao. Hata imekuwa kwamba hao ndio huonekana kuwa vichwa na watumishi wa kweli, kwa kuwa kizazi hiki ni cha mali na pesa.


Hawa ni mfano wa serikali dhalimu iliyowashinda wenye haki kwa nguvu ya udhalimu, nayo ikasimama na kuonesha kuwa udhalimu ndio uungwana na amani na maendeleo na haki. Mtu apingaye udhalimu ule  humsagia meno na kuona kuwa  mtu huyo ndiye hapendi uungwana na amani na maendeleo na haki.


Hata kila mtu mwenye kupenda uungwana na amani na maendeleo na haki inampsasa kuipenda serikali dhalimu ili awe na haki, na mungwana na ili apate amani na maendeleo, lakini mara hayako. Kwa sababu hiyo hujilisha upepo.


  1. MAKRISTO WA UONGO


Neno makristo ni wingi wa neno kristo, na maana ya Kristo ni aliye pakwa mafuta. Hayo mafuta ni ufunuo wa Mungu yaani neno la Mungu. Makristo hawa wanakuwa wa uongo kwa sababu ya ufunuo wao kuwa ni wa uongo.


Katika hawa ushuhuda wa Yesu ambao ndio Roho wa manabii haumo au unakinzana moja kwa moja na Yesu Kristo. Pia ujumbe wao haupo katika kitabu cha ufunuo ambacho ni kitabu cha kila ujumbe na neno litakalokuwepo kutoka kwa Mungu. Maana baada ya Kristo kila mjumbe au mpakwa mafuta na ujumbe wake umeandikwa katika kitabu cha Ufunuo. 


Wapakwa mafuta wa kweli ni kama Paulo (Efeso) na mitume, Irenaeus (Smirna), Martin de tours (Pergamo), Columban (Thiathira), Martin Luther (sardi), John Wesley (Filadelfia), William Seymour(Laodikia), William Branham.


Hawa walipokea ufunuo kwa Mungu, lakini wapakwa mafuta wa uongo ni hao waliojinena wao wenyewe wala ushuda wao haukuwako na haupo, kama Ellen G. White wa SDA, Charles Taze Rusell wa Mashidi wa Yehova, Muhammad wa Waislamu, Joseph smith wa wamormoni au watakatifu wa siku za mwisho, Bahà’u’llah wa wabahà’i na wengine wengi. 


Hizo dini na madhehebu niliyotaja unabii wao wote haupo katika Biblia, kuanzia kanisa la kwanza hata la mwisho, wala baada ya hapo, na shuhuda zao hazina ushuhuda wa Kristo ijapokuwa madhehebu ya SDA na mashahidi wa Yehova wanatumia Biblia lakini kwa ufunuo wa damu na nyama.


ISIKILIZENI SAUTI YA BWANA!


Mawasiliano;

(+255) 0755 251 999.

WASIO HAKI HUNENAJE KWA LUGHA?

HAKUTAKUWA NA UNYAKUO JUU YA KIZAZI HIKI!

THEOLOJIA NI NINI NA KWA NINI HULETA MAUTI?

MANABII NA MAKRISTO WA UONGO. Seh 2

MANABII NA MAKRISTO WA UONGO. Seh 1

        CHANGIA KUPITIA

 

          NMB:       22510119402

          MOBILE: 255755 251 999

​​

             MASHIBE ELIAS NTINGINYA

Mawasiliano:

 

+255 755 251 999

Mbezi, Dar-es salaam

  • Facebook
  • Instagram
  • X
  • TikTok
bottom of page