top of page

NYAKATI YA TANO YA KANISA, SARDI

  • Writer: mashibeelias2
    mashibeelias2
  • 3 days ago
  • 6 min read

Siku ya leo tunatazama nyakati ya tano ya kanisa la Kristo, utakaso wa nne wa kanisa la Kristo. Ni kipindi baada ya kanisa la nne, kuanzia mwaka 1520 BK hadi 1750 BK. Tafsiri ya Sardi ni wale waliotoroka.


Ni ufunuo wa Krito kulisafisha au kulitakasa kanisa la nne, ambalo ni Yezebeli (Katoliki) kutoka katika mafundisho ya wanikolai na mafundisho ya Balaamu. Bwana alilionya toka nyakati ya tatu ya kanisa Pergamo, litubu kwa sababu limefunga ndoa na mafundisho ya balaamu na wanikolai lakini hawakutaka kutubu. Ufunuo huu wa kanisa la sardi ulikuja mahususi kwa ajili ya kuliponya kanisa hili lililokuwa duniani kote yaani katoliki.


Ufunuo wa Yohana 3


¹ Na kwa malaika wa kanisa lililoko Sardi andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye na hizo Roho saba za Mungu, na zile nyota saba. Nayajua matendo yako, ya kuwa una jina la kuwa hai, nawe umekufa.

Habari hizi ziliandikwa kwenda kwa Malaika wa kanisa hili ambaye ni Martin Luther, alikuwa mwalimu wa katoliki ya Urumi (Roman catholic) katika cheo cha Upadre. Martin luther alianza kwa kumridhia mwanamke Yezebeli kama ilivyokuwa kwa Columban, Lakini baadae Martin Luther akashindana na yule mwanamke Yezebeli (Katoliki), akakataa kuridhia mafundisho yake. Akiwa Padre aliandika hoja 95 kupinga mafundisho ya Balaamu na wanikolai ndani ya kanisa. 


Hoja hizi 95 zipo mpaka leo ambazo kimsingi zinapinga mafundisho ya uongo au mafundisho ya wanikolai aliyoyaona martin Luther ndani ya kanisa. Martini Luther hakuhubiri kingine isipokuwa kupinga mafundisho ya wanikolai ndani ya kanisa mpaka ikapelekea kufukuzwa asiwe Padre ndani ya kanisa katoliki ya kiroma (Roman catholic) ambayo ilionekana ndio tawi lenye nguvu na mamlaka ya kidini kuliko ile ya kiothodiksi (Orthodox catholic).


Injili yake ilikuwa ni hukumu ya Mungu juu ya kanisa ambayo aliitaja katika malaika wa kanisa la nne Thiatira, juu ya mwanamke Yezebeli. Turudi nyuma kidogo kuisoma habari hii tena,


Ufunuo wa Yohana 2 


¹⁸ Na kwa malaika wa kanisa lililoko Thiatira andika; Haya ndiyo anenayo Mwana wa Mungu, yeye aliye na macho yake kama mwali wa moto, na miguu yake mfano wa shaba iliyosuguliwa sana.
¹⁹ Nayajua matendo yako na upendo na imani na huduma na subira yako; tena kwamba matendo yako ya mwisho yamezidi yale ya kwanza.
²⁰ Lakini nina neno juu yako, ya kwamba wamridhia yule mwanamke Yezebeli, yeye ajiitaye nabii na kuwafundisha watumishi wangu na kuwapoteza, ili wazini na kula vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu.
²¹ Nami nimempa muda ili atubu, wala hataki kuutubia uzinzi wake.
²² Tazama, nitamtupa juu ya kitanda, na hao wazinio pamoja naye, wapate dhiki kubwa wasipotubia matendo yake;

Mstari wa 21 anasema nimempa mda ili atubu lakini hataki kutubia uzinzi wake (kuachana na mafundisho ya wanikolai na balaam), maana yake onyo hili lilianzia nyakati ya kanisa la tatu Pergamo, wakati mafundisho hayo yanaanza kumea kidogo kidogo kisha katika kanisa la nne thiatira yakawa mafundisho ya kanisa rasimi na ndipo ikatolewa hukumu ambayo ni dhiki kubwa na kutupwa juu ya kitanda yaani kuwa katika maumivu kwa sababu ya kupingwa na Mungu. Martini Luther ni malaika wa Mungu aliyetekeleza adhabu ya Mungu na kuleta maumivu kwa Katoliki.


Pamoja na maumivu, kanisa hili la Katoliki halikukubali kutubu, halikutaka kukubaliana na makosa lililofanya, liliendelea kushika msimamo kuwa mafundisho ya wanikolai na mafundisho ya Balaam ni mafundisho ya Mungu kabisa.


Kitendo cha kutokutubu kwa kanisa hili katoliki yaani Yezebeli, Kinatokana na sababu kuwa Katoliki ilikwisha kufunga ndoa na mme mwingine baada ya kuachana na Mungu. Katoliki hakuishia kuzini tu bali kufunga ndoa na mme mwingine, na katika sheria ya Bwana, hilo halisameheki. Sheria hii aliikumbushia mtumishi wa Mungu Yeremia akisema;


Watu husema, Mtu akimwacha mkewe, naye akienda zake, akawa mke wa mtu mwingine, je! Mtu huyo atamrudia tena? Je! Nchi hiyo haitatiwa unajisi? Lakini wewe umefanya mambo ya ukahaba na wapenzi wengi; nawe, je! Utanirudia mimi? Asema Bwana.”

Yeremia 3:1


Israeli hakumsikiliza nabii Yeremia na sababu ni kuwa walizini na miungu mingine, waliheshimu mafundisho ya uongo kana kwamba ni mafundisho ya Mungu. Kwa sababu hiyo kama sheria ilivyo, mwanamke akiachwa, akaolewa na mwingine; akiachika tena hawezi kumrudia wa kwanza. Na Israeli alimwacha Mungu akaolewa na miungu.


Vivyo hivyo Kanisa lilioana na mafunisho ya balaamu na unikolai katika nyakati ya tatu, Liliolewa na mafundisho ya ibilisi, likakataa kutubu kama lilivyo leo. Halitaki kamwe kumrudia Mungu, halitaki kuachana na hayo mafundisho licha ya kupingwa na Mungu kwa miaka mingi. Na hata leo, Katoliki hajioni kuwa anapigwa na Mungu ili apate kugeuka, bali linadumisha mahusiano wa na yule mme wa pili. Dhehebu hili limepewa sikio la kufa, wasije wakasikia wakaelewa wakaongoka, wakaponywa. Naam, Bwana ametaka sana kuwaponya lakini hawaponyeki. Hivyo Bwana akawageukia waliotoroka kutoka kwa Mwanamke huyu Yezebeli.


Malaika wa kanisa la tatu Martin wa tours na malaika wa kanisa la nne Columban wana tajwa na dhehebu la Katoliki hata leo kuwa ni watakatifu kwa sababu hawakupinga unikolai na ubalaamu ndani ya kanisa. Lakini Martin Luther hayupo katika orodha ya dhehebu lao ijapokuwa alikuwa na daraja la upadre, ni kwa sababu hakuridhia mafundisho yao ya wanikolai.


Tangu wakati ule kanisa hili la katoliki lilitapikwa kama taka za fedha. Likawa dhehebu tangu wakati ule hata leo. Yaani ni dongo la fedha lililokataa kuyeyushwa ili uchafu uondolewe na fedha ipatikane. Ni martin luther na wale waliomfuata ndio walio fedha iliyopatikana kwenda hatua inayofuata ya kusafishwa, ambao nao katika makanisa mawili yanayofuata tutaona wakiwa na roho ile ile kutokutaka kutubia makosa yao.


UNA JINA LA KUWA HAI NAWE UMEKUFA.


Pamoja na uthubutu wa Martin luther kuwapinga watu wa nyumba moja na yeye yaani wakristo wenzake, huduma yake haikufikia lengo, haikufikia utilimilifu wa kuondoa hayo mafundisho ya wanikolai, balaam na Yezebeli. Aliondoa mafundisho ya uongo baadhi na mengine akaondoka nayo kama mafundisho halali kwake. Mfano ubatizo wa watoto, ubatizo wa kunyunyizia, Kuendelea kuomba wafu, kuheshimu uungu wa Mariamu. Kuendelea kutegemea neema ya Mungu itawasafisha dhambi yenyewe wala si kwa matendo.


Kwa sababu hizo alikuwa bado ni mfu katika roho licha ya kuwa analo jina la Kristo. Injili yake bado ilibaki na unikolai na ubalaamu, haikung’oa kila pando la ibilisi. Hivyo kusudi la injili la kufikilia utakatifu likawa gumu bado.


Dhehebu la Martin Luther ambalo wanajulikana kama walutheri (lutherans) leo, watu waliotokana na Luther ni watu walio na jina lililo hai lakini bado wamekufa. Naam, walitolewa katika dhehebu la katoliki ambalo limekufa katika roho ili wasife kwa yale mafundisho ya wanikolai, lakini wangali katika mauti ile ile. Ajabu ni kuwa wanasubiri unyakuo.


Bwana anaendelea kusema na martin luther pamoja na walutheri wote kuwa;


² Uwe mwenye kukesha, ukayaimarishe mambo yaliyosalia, yanayotaka kufa. Maana sikuona matendo yako kuwa yametimilika mbele za Mungu wangu.
³ Basi kumbuka jinsi ulivyopokea, na jinsi ulivyosikia; yashike hayo na kutubu. 

Kitu pekee ambacho kingeweza kumfanya martin Luther ayajue yaliyosalia, ambayo hakuyaondoa ni kukesha. Na kukesha huko sio kukesha usiku bali kuongeza bidii ya kupokea ufunuo wa Mungu. Ikiwa hataondoa hayo mafundisho atavuna mabua ndani ya kanisa. Lakini Martin Luther hakukesha, yaani Yeye na kanisa kwa sababu yaliyosalia yalisalia na neno la Mungu likazidi kudumaa ndani ya kanisa la Kristo alilokomboa kwa njia ya martin Luther kutoka mauti aliyoitupa Bwana kwa kanisa lote yaani Katoliki (Catholic).


Walakini usipokesha, nitakuja kama mwivi, wala hutaijua saa nitakayokuja kwako.


Bwana alikuja kwake pia kama mwizi anayekuja kuiba, hapigi hodi, haingilii mlangoni. Maana yake Kristo alikuja kwa njia ya ufunuo mwingine kumpinga yeye naye kwa sababu ya mafundisho ya uongo ya wanikolai na balaamu na yezebeli aliyotoka nayo katoliki.


Jambo hili utaliona baada ya uamsho mkubwa alioufanya martin Luther wakiitwa wa-protestant yaani wapingaji wa katoliki, kulitokea kupingwa kwa mafundisho yake pia na walimu wengi kama wakina John Calvin, Servato, John smyth, Jacob ammann, Menno Simons n.k, na hatimaye ufunuo kamili ukaja kwa njia ya malaika wa sita ambaye tutamwona katika kanisa la Sita.


⁴ Lakini unayo majina machache katika Sardi, watu wasioyatia mavazi yao uchafu. Nao watakwenda pamoja nami hali wamevaa mavazi meupe, kwa kuwa wamestahili.
⁵ Yeye ashindaye atavikwa hivyo mavazi meupe, wala sitalifuta kamwe jina lake katika kitabu cha uzima, nami nitalikiri jina lake mbele za Baba yangu, na mbele ya malaika zake.

Kutokana na makosa hayo, Martin Luther na waliomwamini walipaswa kutubu, lakini pia walikuwako watu ambao hawakukuabaliana na mafundisho ya wanikolai hata yale aliyokuwa nayo Martin Luther, wakajitenga naye kama makanisa ya Anabaptist, mennonites, na Amish. Hawa ndio majina machache katika sardi wasiotia mavazi yao uchafu.


⁶ Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa.

Mawasiliano;

+255755251999

 
 
 

Recent Posts

See All
NYAKATI YA SABA YA KANISA, LAODIKIA

NYAKATI YA SABA YA KANISA, LAODIKIA. Kanisa la Laodikia ni nyakati kuanzia 1906 BK hata leo. Katika makanisa sita tuliyotoka kutazama, tumeona habari ambazo zinafanya ujue kanisa lilikopitia mpaka hap

 
 
 
NYAKATI YA SITA YA KANISA, FILADELFIA

Tumetoka kuona jinsi kanisa la tano au nyakati ya tano ya kanisa ambapo Katoliki (roman catholic na orthodox catholic) waliitwa kutubu, lakini walikataa kutubu ili watakaswe kwa lile neno la Mungu. Nd

 
 
 
NYAKATI YA NNE YA KANISA, THIATIRA

Yezebeli alikufa miaka mingi kabla ya maneno haya ya kitabu cha ufunuo kuandikwa, hivyo mwanamke huyu hana uhusiano wowote na kilichoandikwa, lakini Yezebeli anayezungumziwa hapa ni kanisa. Kwa sababu

 
 
 

Comments


bottom of page