NYAKATI YA NNE YA KANISA, THIATIRA
- mashibeelias2

- Nov 15, 2025
- 6 min read
Updated: Dec 22, 2025
KANISA LA NNE, THIATIRA
Hiki ni kizazi cha nne cha kanisa ambacho kinaanzia mwaka 606 BK hadi 1520 BK. Ni ufunuo wa kulitakasa kanisa la tatu ambao unazaa kanisa la nne. Tusoma habari hizi katika ufunuo wa Yohana 2:18-29
¹⁸ Na kwa malaika wa kanisa lililoko Thiatira andika; Haya ndiyo anenayo Mwana wa Mungu, yeye aliye na macho yake kama mwali wa moto, na miguu yake mfano wa shaba iliyosuguliwa sana.
Kristo anajitambulisha kwa malaika huyu kuwa yeye ni mwana wa Mungu, macho kama mwali wa moto, miguu iliyosuguliwa sana, ikimaanisha macho yake yana hasira kwa kile yanachoona. Miguu yake yaani hatua zake ni takatifu/safi kama shaba ilisuguliwa sana. Tafsiri yake ni kuwa hatua za Malaika huyu zilikuwa safi na takatifu lakini hazikufikia kiwango kinachotakiwa.
Ujumbe wa Mungu kwa kanisa hili uliletwa na malaika Columban, huyu alikuwa mmisionari wa injili katika mataifa kama Ireland, Uswizi, Italia na Ufaransa. Aliendeleza utamaduni wa kujenga na kukaa katika monasteri (nyumba za watawa) kama malaika aliyemtangulia ‘Martin wa tours’, utaratibu ambao kipindi kile ulimfanya mtu aishi uhalisia wa injili ya Kristo.
PONGEZI
¹⁹ Nayajua matendo yako na upendo na imani na huduma na subira yako; tena kwamba matendo yako ya mwisho yamezidi yale ya kwanza.
Hapa kuna mambo manne yaani Upendo, Imani, huduma na subira yanayomtambulisha Columban, mambo haya alifanya katika kiwango kikubwa. Upendo huu sio mwingine isipokuwa upendo wa kumpenda Mungu, kulicha neno lake. Columban alidhihirisha imani na matendo makuu katika kizazi chake. Alitenda miujiza mingi na kila wakati aligombana na wafalme anakokaa baada ya kuwapinga katika uovu wao.
Alizidi kukua katika mambo yote haya (upendo, imani, huduma na subira) hata matendo yake ya mwisho yalikuwa bora zaidi kuliko mwanzo, hakuwa vuguvugu bali moto ulizi kuongezeka kadiri siku zinavyokwenda mbele. Hakuogopa mwandamu juu ya neno la Mungu.
ONYO
²⁰ Lakini nina neno juu yako, ya kwamba wamridhia yule mwanamke Yezebeli, yeye ajiitaye nabii na kuwafundisha watumishi wangu na kuwapoteza, ili wazini na kula vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu.
²¹ Nami nimempa muda ili atubu, wala hataki kuutubia uzinzi wake.
Pamoja na upendo, imani, huduma na subira; mambo yaliyompa utukufu mbele za Mungu, Mwana wa Mungu anasema, ana neno juu ya malaika huyu Columban analolichukia kwake, ni kile kitendo cha kumridhia mwanamke Yezebeli. Kumridhia maana kukubaliana nae au kufuata matakwa yake.
HUYU MWANAMKE YEZEBELI NI NANI?
Mwanamke huyu alitokea katika nchi ya Israeli takribani miaka 850 Kabla ya Kristo, alikuwa mke wa Ahabu mfalme wa Israeli lakini asili yake alikuwa Msidoni ikijulikana kama Lebanoni kwa leo. Aliabudu mungu baali. Yezebeli alifanikisha kuwageuza Israeli wamtumikie mungu baali badala ya Mungu, Yezebeli alikuwa mwerevu kama nyoka alivyomhadaa Hawa, naye akawahadaa watumishi wa Mungu kuenenda kwa fumbo za Yezebeli kumwabudu baali.
Yezebeli alikufa miaka mingi kabla ya maneno haya ya kitabu cha ufunuo kuandikwa, hivyo mwanamke huyu hana uhusiano wowote na kilichoandikwa, lakini Yezebeli anayezungumziwa hapa ni kanisa. Kwa sababu Mwanamke hufunua kanisa, dhehebu au dini fulani. Hivyo Columban alilidhia mafundisho ya kanisa ambalo linaenda kwa mafundisho kama yale ya Yezebeli, kuwafanya watu walioacha dhambi wairudie dhambi kana kwamba ni kumheshimu Mungu.
Ni mafundisho kama ya Balaam, na kama ya nyoka au wanikolai ambayo yanakufanya kile kilichokatazwa na Bwana Mungu ukakitende hicho hicho. Tafsiri yake neno la Mungu/Kristo linakufa ndani ya mtu, naye anabaki na kitabu kilichoaandikwa maneno ya Mungu ambayo huyo anayekibeba anapingana nayo bila kujua.
Mwanamke huyu au kanisa hili aliloliridhia
Columban ni lile lile la Kristo lakini katika kizazi cha tatu (Kanisa la Pergamo), malaika wa kizazi kile (Martin wa tours) alionywa kuwa anao watu huko walio na mafundisho ya Balaamu, na ya wanikolai. Liliambiwa litubu na kama halitatubu Kristo atakuja na kufanya vita dhidi yake. Tujikumbushe maneno hayo;
Ufunuo wa Yohana 2
¹² Na kwa malaika wa kanisa lililoko Pergamo andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye na huo upanga mkali, wenye makali kuwili.
¹³ Napajua ukaapo, ndipo penye kiti cha enzi cha Shetani; nawe walishika sana jina langu, wala hukuikana imani yangu, hata katika siku za Antipa shahidi wangu, mwaminifu wangu, aliyeuawa kati yenu, hapo akaapo Shetani.
¹⁴ Lakini ninayo maneno machache juu yako, kwa kuwa unao huko watu washikao mafundisho ya Balaamu, yeye aliyemfundisha Balaki atie ukwazo mbele ya Waisraeli, kwamba wavile vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na kuzini.
¹⁵ Vivyo hivyo wewe nawe unao watu wayashikao mafundisho ya Wanikolai vile vile.
¹⁶ Basi tubu; na usipotubu, naja kwako upesi, nami nitafanya vita juu yao kwa huo upanga wa kinywa changu.
Naam, onyo hili halikutendewa kazi, uovu ukazidi kushinda, ndipo katika kanisa hili la nne anaporudia kusema;
²¹ nami nimempa muda ili atubu, wala hataki kuutubia uzinzi wake.
Sasa hapa ndipo imewekwa wazi kuwa kanisa la tatu halikutubu, na mafundisho hayo ya Balaamu, na wanikolai yamekuwa mafundisho si ya watu wachache bali ya kanisa zima ambalo Columban hakupingana nalo kwa habari ya mafundisho hayo, yeye mwenyewe aliyaridhia mafundisho ya Balaamu na yale ya wanikolai ndani ya kanisa ijapokuwa kwa sehemu kubwa hakukaa kanisani bali katika nyumba za watawa waliojitenga mbali na kanisa.
Na utakatifu wao ulikuwa wa juu sana kulinganisha na kanisa. Watawa wa kipindi kile sio watawa wanaoonekana leo katika dhehebu la katoliki. Hawa wa leo wanafanya kama kuigiza utawa na kwa sababu ya sheria ya dhehebu lao.
Pamoja na sheria za kitawa alizokuwa amezitunga Columban kuwafanya waishinde dhambi, bado aliendelea kuheshimu mafundisho ya wanikolai ndani ya kanisa. Mfano mzuri katika safari yake kutoka Ireland kwenda Gaal (ufaransa kwa leo), alipita katika kaburi la martin de tours kwa ajili ya kumwomba martin wa tours kutokana na fundisho la wanikolai la kuomba wafu wakusaidie au wakuombee kwa Mungu.
HUKUMU JUU YA KANISA HILI (YEZEBELI).
²² Tazama, nitamtupa juu ya kitanda, na hao wazinio pamoja naye, wapate dhiki kubwa wasipotubia matendo yake;
²³ nami nitawaua watoto wake kwa mauti. Na makanisa yote watajua ya kuwa mimi ndiye achunguzaye viuno na mioyo. Nami nitampa kila mmoja wenu kwa kadiri ya matendo yake.
Kanisa hili ambalo mafundisho yake ni kwa mfano wa Yezebeli, ndio dhehebu la katoliki. Na tafsiri ya thiatira ni mwanamke anayetawala, na huyo mwanamke ni Katoliki (Yezebeli) ambalo lilikuwa kanisa moja tangu mitume. Katoliki imetokana na kitohozi cha neno la kiingereza CATHOLIC, tafsiri yake ni dunia nzima au kote duniani. Ilikuwa kipindi hiki kanisa lilikuwa limeunganika kiutawala kote duniani.
Mwanamke huyu yaani kanisa katoliki (Yezebeli) alitawala mpaka wakati wa martin Luther, ambaye alileta ile hukumu ya Mungu juu yake na kumfanya atapikwe na Bwana hata leo. Ijapokuwa angali yupo hata leo na ukahaba ule ule na hata zaidi lakini Mungu aliachana na Katoliki na kwenda na waprotestanti waliozaliwa na martin Luther kisha baadae wapentekoste. Leo hii Katoliki ni dongo la fedha (ores) yaani waliokata kutubu.
Mafundisho ya Balaam, wanikolai, na Yezebeli yanaishi ndani ya Katoliki hata leo. Na Yezebeli hii (katoliki) iligawanyika kulingana na utawala wa kirumi mwaka 1054 BK na kuwa katoliki ya kiroma na kiothodoksi au katoliki ya magharibi(roman catholic) na katoliki ya mashariki (orthodox catholic).
Mwana wa Mungu yaani Yesu anasema atalitupa kanisa hili juu ya kitanda wapate dhiki kubwa wasipotubia matendo yao! Maana yake mpaka katika nyakati ya kanisa la nne walikuwa na mda wa kutubu bado. Na kipindi cha kanisa hili ni takribani miaka 1000, Ni kipindi kirefu cha giza katika kanisa Bwana akingoja watubu.
Kanisa hili katoliki ndio dhehebu la kwanza kuwepo, ni baada ya kukataa kutubu ili wapate kutakaswa juu ya uongo wao. Walimu wake hawakumpokea columban, ijapokuwa hakuwapinga mafundisho yao, lakini hawakumfurahia, walimnung’unikia na hata kumpinga na pia kupinga utaratibu wake wa kitawa aliouanzisha. Alikuwa na maadui wengi ambao ni mapadre, maaskofu n.k. ndani ya kanisa kuliko maadui wa ulimwengu.
Msitari wa 23 anaendelea kusema atawaua watoto wao yaani watoto katika roho watakaozaliwa kwa mafundisho hayo ya uongo. Na makanisa yote yaani habari zile kanisa la saba (kizazi hiki) watazijua pia.
²⁴ Lakini nawaambia ninyi wengine mlioko Thiatira, wo wote wasio na mafundisho hayo, wasiozijua fumbo za Shetani, kama vile wasemavyo, Sitaweka juu yenu mzigo mwingine.
²⁵ Ila mlicho nacho kishikeni sana, hata nitakapokuja.
Kisha Neno la Kristo linakwenda kwa baadhi ya watu ambao bado walikuwa hawajasikiliza mafundisho ya balaamu na wanikolai; watu ambao walikuwa hawajazisikiliza fumbo za shetani zinazo wageuza akili na kuwafanya waigeukie dhambi. Fumbo za shetani ni fasiri zenye kuondoa amri ya Mungu, zinatoa fasiri zinazo halalisha kufanya yale yaliyokatazwa.
Mfano utaona Musa na manabii wote wanaagiza kutochonga sanamu na kuisujudia au kuitumikia, Lakini dhehebu la katoliki limechonga picha za Maria na Yesu na wanasujudu mbele yake ili kuzipa heshima, kuomba, au kuomba ziwaombee n.k, utajiuliza jambo hili liliwezekanaje kuingia kanisani? Fumbo za shetani ndio hasa zimetenda kazi hiyo.
Mfano mwingine katika kizazi hiki cha saba utaona mwanamke akihutubu katika makanisa ya wapentekoste wanaosema tunafuata injili ya mitume, lakini mtume Paulo alisema kwa maagizo ya Roho mtakatifu kuwa simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha, lakini leo ni walimu na wachungaji kwa sababu ya fumbo za shetani.
²⁶ Na yeye ashindaye, na kuyatunza matendo yangu hata mwisho, nitampa mamlaka juu ya mataifa,
²⁷ naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, kama vyombo vya mfinyanzi vipondwavyo, kama mimi nami nilivyopokea kwa Baba yangu.
²⁸ Nami nitampa ile nyota ya asubuhi.
Kisha imetajwa zawadi kwa washindi ambao watayatunza matendo ya Kristo, yaani mwenendo wa Yesu Kristo, wale ambao hawaendi katika ufunuo wa nyoka, wale ambao hawaridhii mafundisho ya Yezebeli yaani Katoliki (Roman na orthodox).
Yeye atakayeyatunza matendo ya Kristo hata ufunuo wa tano atapewa mamlaka juu ya mataifa, naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, atawaponda kama vyombo vya chuma vipondwavyo. Na huyu aliyeshinda ni Martin luther ambaye tutakuja kuona habari zake katika kanisa linalofuata. Hakumridhia huyu mwanamke Yezebeli, alileta vita dhidi yake isiyo ya kawaida.
²⁹ Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa.
Mawasiliano:
+255 755 251 999



Comments