top of page

KUPATWA KWA MWEZI HUMAANISHA NINI KATIKA ROHO?

  • Writer: mashibeelias2
    mashibeelias2
  • Sep 8
  • 3 min read

Jana tarehe 7 ya mwezi huu wa 9, 2025 limeonekana tukio la nadra sana kutokea, mwezi ulikuwa kama damu. Tukio hili huitwa kupatwa kwa mwezi (lunar eclipse), yaani dunia inakuwa katikati ya jua na mwezi. Hivyo mwezi unakuwa kwenye kivuli cha dunia.


Dunia yetu ipo katika tabaka mbili, tabaka la anga na tabaka la ardhi. Wakati dunia inalikabili jua upande wa anga, dunia inakuwa kwenye nuru na wakati dunia inapolikabili jua upande wa ardhi dunia inakuwa kwenye giza upande wa anga, na giza hilo tunaliita usiku. Yaani ardhi inaliziba jua na kivuli chake kinakuwa ndio usiku kwetu. Kwa lugha rahisi dunia inakuwa imeuziba mwezi usipate nuru ya jua. Nimetumia lugha ambayo kila mtu anaweza kuelewa.

Kupatwa kwa mwezi, mwezi ukiwa mwekundu
Kupatwa kwa mwezi, mwezi ukiwa mwekundu

NINI MAANA YAKE KATIKA ROHO?


Tukio hili halina maana yoyote katika roho, haliongezi wala kupunguza chochote wala kuonyesha ishara iwayo yote katika roho, kwamba ni ishara mbaya au nzuri. Ni tukio la kawaida kabisa, kama tu mwezi au jua linavyozama na kuchomoza, au mvua kunyesha miezi fulani na si miezi fulani. Lakini kwa waabudu sanamu tukio hili hulivisha uungu fulani, wengine huamini ni ishara ya mambo mabaya, na wengine huamini ni ishara ya mambo mazuri hata hutii sheria fulani ili mambo mazuri yawapate au mambo mabaya yasiwapate au yasitokee; na hata wengine hukusanyika kuomba mungu wao (miungu) ili wasipate madhara waliojitungia kwamba yatawapata.


Matukio kama haya miungu ya zamani ambayo hata leo mingine ipo waliamini ni ndoa kati ya jua na mwezi, wengine waliamini miungu yao imekasirika, hivyo inalimeza jua na mwezi, wengine waliamini ni kufa na kuzaliwa kwa jua, hivyo ni ishara nzuri kwao wanasherekea kila wakati wa tukio hilo.


Narudia tena, hakuna ishara yoyote katika roho na ikiwa utafanya ama kutii sheria yoyote kuhusu kupata au kutopata jambo fulani, basi ujue unatumikia miungu na hiyo ndio dhambi iliyo kubwa, maana imeandikwa mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote, maana yake uichukie miungu kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote. Lakini tukio hili lielewe kwa namna ya mfano wa ufalme wa Mungu.


UFALME WA MBINGUNI UNAFANANA NA KUPATWA KWA MWEZI.


Tukio hili ni mfano wa ufalme wa mbinguni kama jinsi ambavyo Kristo alitolea vitu kama mbegu, miti, biashara kuelezea ufalme wa Mungu, wala vitu hivi havina maana yoyote katika roho bali kwa kuvitazama unapata ufunuo wa ufalme wa Mungu.


Hapa nataka tuone tukio hili jinsi linavyoelezea ufalme wa Mungu. Mwezi huwakilisha kanisa, maana yake mwezi hauna nuru yake wenyewe isipokuwa huakisi kutoka katika jua. Ndivyo na kanisa, halina neno lake lenyewe isipokuwa limepata kutoka kwa Mungu yaani ufunuo utokao kwa Mungu (Mathayo 16:17).


Jua lina nuru yake lenyewe wala halitegemei sehemu nyingine kama ilivyo kwa Mungu, hafundishwi wala kujifunza mahali ili apate kuamua. Kama mwezi unavyoizunguka dunia kuipa nuru wakati wa giza, na nuru si yake bali umeakisi katika jua, ndivyo na kanisa lilivyo katika mzunguko ulimwenguni kuupa nuru ya Mungu.


 Hivyo kwa kifupi,

  1. MWEZI ni kanisa

  2. JUA ni neno litokalo kwa Mungu,

  3. DUNIA ni ufunuo utokanao na damu na nyama, yaani wanadamu (theolojia). (Mathayo 16:17).


Kwa maana hiyo kupatwa kwa mwezi, ambapo mwezi unakuwa katika kivuli cha dunia yaani dunia inakuwa imeuziba mwezi usipate nuru ya jua ni kanisa linapokuwa limezibwa na mafundisho yatokanayo na dunia yaani theolojia za wanadamu, mapokeo ya wanadamu na linakuwa haliwezi kupokea ufunuo utokao kwa Mungu.

3

Kanisa linakuwa katika giza, kwa sababu halina Nuru ya Mungu, theolijia ambazo ni ufunuo wa damu na nyama, maagizo ya wanadamu ndio zinakuwa kiongozi wa kanisa. Ndio zinakuwa Mungu kwa kanisa, ndio zinakuwa Yesu kwa kanisa. Ndivyo ulivyo ufalme wa Mungu katika nyakati hizi.

Jinsi gani Bwana Mungu alituma manabii nyakati zile wakiwa na ufunuo wa Mungu ili kuleta nuru kwa kanisa lile, lakini giza yaani theolojia, zikashindana nao na kuwashinda, wakauwawa na mafundisho ya wanadamu yakaendelea hata wakati wa Kristo ambaye aliyashinda, ijapokuwa yalirudi tena baada ya Kristo hata leo.


Kwa wewe uliyeuona mwezi umekuwa mwekundu kama damu, ndivyo na madhehebu yalivyo, mafundisho yake yanaleta mauti, yanamwaga damu za wale waliokuwa na uzima kwa kumwamini Yesu Kristo na kubatizwa, yanaangamiza kilicho okolewa.


Maana madhehebu yote baba yao ni mmoja, naye ni ibilisi aletaye mafundisho ya kuwafanya watu walioacha dhambi wairudie dhambi, walioichukia dhambi waipende dhambi, waliouchukia ulimwengu waupende ulimwengu. Madhehebu hutwaa yaliyo ya ibilisi na kuyaweka kanisani na yale ya Mungu huyaondoa ili waweke ya ibilisi. Kama jinsi ibilisi alivyomtenza nguvu Adamu na Hawa, ndivyo na kanisa leo lilivyo. Mwenye masikio na asikie!


Mawasiliano

 
 
 

Recent Posts

See All
NYAKATI YA PILI YA KANISA, SIMIRNA.

Leo tunatazama kanisa la pili baada ya Efeso, yaani nyakati ya pili ya kanisa. Au kutakaswa kwa kanisa la kwanza. Kumbuka kanisa la kwanza liliacha upendo wa kwanza, lakini pia watu wale mbali na mala

 
 
 
NYAKATI YA KWANZA YA KANISA, EFESO.

Ndipo kwa sababu hiyo aliuacha upendo wa kwanza, alikuwa sahihi kabisa kumkemea Petro, na kila alichokuwa anakifanya lakini naye akaanza kupoa mwishoni mwa huduma yake kama Petro. Akachukuliana na wab

 
 
 

Comments


bottom of page