KALAMU YA UONGO YA WAANDISHI IMEIFANYA BIBLIA KUWA UONGO
- mashibeelias2

- Aug 9
- 3 min read
Updated: Aug 23
Shalom, Karibu katika Neno la Mungu, na moja kwa moja tusome maandiko katika Yeremia 8
8 Mwasemaje, Sisi tuna akili, na torati ya Bwana tunayo pamoja nasi? Lakini, tazama, kalamu yenye uongo ya waandishi imeifanya kuwa uongo.
Takribani miaka 600 kabla ya Kristo, Yeremia alihubiri Neno la Mungu katika Israeli ili wamrudie Mungu wao. Lakini hawakujua wamemwacha lini hata wamrudie, kwa sababu torati walikuwa nayo wakiisoma na kufundishwa kila siku ya sabato kama torati ilivyoagiza. Hivyo ilikuwa vigumu kumgeukia mtu huyu aliyeitwa Yeremia ama nabii awaye yote.
Ndipo Yeremia kwa kulijua hilo aliwaambia, mwasemaje, kwamba tuna akilia na torati ya Bwana tunayo pamoja nasi, Lakini kalamu ya Uongo ya waandishi imeifanya torati kuwa uongo.
KALAMU YA UONGO YA WAANDISHI NI NINI?
Kalamu unaifahamu, kazi yake ni kunakili mawazo ya mtu au ya Mungu kuwa katika maandishi. Kama ambavyo torati ni mawazo ya Mungu yaliyonakiliwa na Musa Mtumishi wake, basi ilikuja torati nyingine ya pili, wala si ya pili bali ile ya Mungu ilifanywa kuwa uongo. Kalamu ya uongo ya waandishi ni fasiri za maandiko ambazo ni za uongo, ni ufunuo wa damu na nyama yaani ufunuo usiotoka kwa Mungu.
Sasa tafsiri hizi kadiri zinavyozaliwa na kuongezeka, huimeza tafsiri ya kweli au maana halisi ya lile andiko, maandiko na hata torati au Biblia kwa ujumla. Ndipo hapo Yeremia anaposema kalamu ya uongo ya waandishi imeifanya torati kuwa uongo. Maana yake tafsiri za uongo, ufunuo wa damu na nyama ndio umewekwa madhabahuni unafuatwa na kanisa lote. Na watu wote huinama na kusujudi mbele ya ule uongo.
Kalamu za uongo ambazo ni tafsiri za uongo zinaweza kuwa zimeandikwa au zikawa zinafundishwa kwa matamshi pekee, yote ni mamoja.
Ndipo kwa kutofautiana na kukua zinaunda majina kama yale ya mafarisayo, masadukayo n.k. Katika nyakati hizi za leo ni majina ya madhehebu unayoyaona, ambayo kila moja lina theolojia yake yaani kalamu yake lililojiandikia kutoka katika biblia. Maana yake hakuna dhehebu lisemalo kweli ya Mungu bali kila moja huenenda na kufundisha kulingana na kalamu yao ya uongo.
Katika kipindi cha Bwana Yesu, Si mafarisayo, wala masadukayo, wala waesene, ama wazelote; madhehebu ya kipindi kile aliyekuwa na kweli ya Mungu, ndipo wote walithibitika kuwa na kalamu za uongo kwa lile neno la Kristo.
Katika nyakati hizi zipo kalamu nyingi na za kila aina, na hata tafsiri halisi ya Neno la Mungu katika Biblia imetoweka na kubaki hizi kalamu za uongo. Na hapa ndipo Neno la Mungu kwa njia ya nabii Amosi linatimia;
Amosi 8:11
Angalia, siku zinakuja, asema Bwana MUNGU, ambazo nitaleta njaa katika nchi; si njaa ya kukosa chakula, wala kiu ya kukosa maji, BALI YA KUKOSA KUYASIKIA MANENO YA BWANA.
Njaa hii ilikuwepo kipindi kabla ya Yohana mbatizaji na Yesu Kristo, kizazi kile kilizungukwa na tafsiri za uongo kiasi cha kulifanya Neno la Mungu life katikati ya jamii ile zikabaki kalamu za uongo. Hata Bwana Mungu alipolisimika tena Neno lake, kwanza kwa njia ya Yohana na kisha Yesu Kristo.
Ndipo waliokuwa na njaa wakaja kutwaa chakula na maji kwao. Njaa hii ipo nyakati hizi yaani sasa, tena njaa kuu.
Kumbuka! Njaa hii haipo kwa kila mtu, bali wale wenye kiu na haki, wenye kulitafta Neno la Mungu. Kwa sababu kila mwenye kuishi kwa ajili ya chakula huona njaa kisipokuwepo kile chakula, vivyo hivyo na kila mwenye kuishi kwa ajili ya Neno la Mungu huona njaa lisipokuwepo.
Hivyo Neno la Mungu lisipokuwepo, walio kinyume na Bwana hustawi kwa kuwa chakula chao kipo tele, ambacho ni mafundisho ya uongo.
Lakini pasipo Neno la Mungu huja njaa kwao walio upande wa Mungu. Basi hao walio upande wa Mungu ndio ile ngano na walio kinyume ndio yale magugu (Mathayo 13:24-43), yote mawili yamemea katika shamba moja yaani kanisa. Nayo sharti yatengwe, naam, Laodikia na alie sasa!
Maana shoka limekwisha kuwekwa katika shina lake. Sauti ya Bwana imekuja ili kung'oa kila ambalo hakulipanda na kutwaa yaliyo yake. Naam, laodikia na aseme!
Ijapokuwa Laodikia amenenepa atakonda kwa kukosa chakula. Bwana atang'oa uongo wako wote uliojinena na kusema 'mimi ni tajari sina haja na kitu kingine' atakausha visima ulivyovichimba upate kuweka akiba ya maji, na kwa kiu utazimia na uzima utakutoka.
La mkighairi kwenenda katika uongo wenu, Nitawapa chakula na maji ya uzima asema Bwana!

Tazama pia kwa njia ya video Juu ya laodikia.
Basi kwa kuwa umelisikia Neno hili kwa njia ya mtandao. Unaweza Kulifikia kwa njia hii;
+255755 251 999

Comments