top of page
“KWA KUWA UMELISHIKA NENO LA SUBIRA YANGU, mimi nami nitakulinda, utoke katika saa ya kuharibiwa iliyo tayari kuujilia ulimwengu wote, kuwajaribu wakaao juu ya nchi.”

Ufunuo wa Yohana 3:10.


Karibu kila jambo linahitaji subira, na subira ni uvumilivu katika kungoja ahadi au kukamilika kwa jambo husika. Mfano mwanamke anahitaji kusubiri miezi tisa baada ya ujauzito kutungwa mpaka kujifungua. Katika kipindi chote cha miezi tisa atapitia masumbufu mengi na baada ya miezi tisa atapata mtoto maana ndio alichokuwa anasubiri. Mkulima vile vile, akipanda mbegu katika shamba anahitaji subira ya miezi kadhaa kupata mazao maana ndio anayotazamia. 


Hekima hii haijatoka kwa wanadamu bali kwa Mungu. Yeye ndiye aliyeweka mda wa miezi tisa wa kubiri hata mtoto azaliwe. Vivyo hivyo anayo subira Yeye mwenyewe katika mambo mbambali ayatendayo, na moja wapo ni subira ya neno lake. Bwana Mungu amepanda mbegu katika ulimwengu yaani neno lake ili apate mavuno wakati wa mavuno utakapowadia.


Na kwa sababu hiyo, amesubiri kwa miaka mingi na vizazi vingi akifanya kazi katika shamba ili litoe mavuno mengi na yaliyo bora. Na mavuno hayo mazuri na bora ni haya;


Mathayo 5


⁴⁸ Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.

Jumla ya maneno ya Mungu, aliyoyasema, anayoyasema na atakayoyasema ni kuwafanya watu wawe wakamilifu kama yeye alivyo mkamilifu. Hivyo subira ya Mungu baada ya kupanda neno lake ni kuona watu waliolipokea wanakuwa wakamilifu kama Yeye.


Katika vizazi saba ambavyo Mungu ameliijilia kanisa kwa neno lake, ni kizazi cha sita ndio kilimpendeza Bwana. Kiliishi lile neno la subira yake yaani utakatifu. Neno la Mungu kwa nia ya John Wesley lilijikita katika utakatifu, naye Bwana alisifu kanisa lile kwa sababu amepata kile alichokuwa anakisubiri. Haya ndiyo maneno ya Bwana;


Ufunuo wa Yohana 3


⁷ Na kwa malaika wa kanisa lililoko Filadelfia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye mtakatifu, aliye wa kweli, aliye na ufunguo wa Daudi, yeye mwenye kufungua wala hapana afungaye, naye afunga wala hapana afunguaye.
⁸ Nayajua matendo yako. Tazama, nimekupa mlango uliofunguliwa mbele yako, ambao hapana awezaye kuufunga, kwa kuwa unazo nguvu kidogo, nawe umelitunza neno langu, wala hukulikana jina langu.
⁹ Tazama, nakupa walio wa sinagogi la Shetani, wasemao kwamba ni Wayahudi, nao sio, bali wasema uongo. Tazama, nitawafanya waje kusujudu mbele ya miguu yako, na kujua ya kuwa nimekupenda.
¹⁰ KWA KUWA UMELISHIKA NENO LA SUBURA YANGU, mimi nami nitakulinda, utoke katika saa ya kuharibiwa iliyo tayari kuujilia ulimwengu wote, kuwajaribu wakaao juu ya nchi.

Ujumbe wa John Wesley ulikuwa kuwafanya watu wawe wakamilifu mbele za Mungu. Ujumbe wake ulikuwa unaosha kikombe kwa ndani, haukua sawa na ujumbe wa wapentekoste (walokole) waolikuja baada yake, maana hawa walikuja na ujumbe wa kuosha kikombe kwa nje.


Ujumbe wa walokole waliozaliwa kwa ujumbe wa William Seymour, umejikita kumfunika mtu asiye mtakatifu vazi la utakatifu ili aonekane ni mtakatifu wakati sio. Hapa utaona mafundisho kuwa ukizaliwa mara ya pili umekuwa mtakatifu. Hatuishi kwa sheria bali kwa neema n.k.


Wapentekoste humaanisha ukitupa mbegu ya mahindi katika udongo, ifukue mara, itakuwa tayari kwa mavuno. Wakiisha kupanda huitoa mbegu walioipanda ili iwe mavuno; kwamba mavuno na kupanda ni sawa. Ndio maana kwa nini Bwana alipendezwa na Kizazi cha sita na kuchukizwa na kizazi cha saba. Kizazi cha saba kwa vinywa vyao wanaelekea mbinguni na kwa matendo yao wanaelekea kuzimu.


Ufunuo wa Yohana 3


¹⁴ Na kwa malaika wa kanisa lililoko Laodikia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye Amina, Shahidi aliye mwaminifu na wa kweli, mwanzo wa kuumba kwa Mungu.
¹⁵ Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto.
¹⁶ Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu.
¹⁷ Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi.
¹⁸ Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona.
¹⁹ Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu.
²⁰ Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.

Kizazi cha saba amekinena kuwa ni vuguvugu, tena kitubu kutoka katika uvuguvugu. Maana yake neno la subira ya Mungu kwa kanisa la saba lipo kama halipo. Ni watu ambao wameridhika katika kuhesabiwa haki kwa imani, wala hawaendi katika ukamilifu badala yake wanataka kuamini watahesabiwa kuwa wakamilifu kwa imani.


Kile anachokisema kuwa si moto wala si baridi, ni kulingana na subira yake. Anatazamia kuona ukamilifu lakini anaona watu ambao wasema tayari sisi ni wakamilifu, kimatendo na kimaarifa. Ndio maana hawana haja na kitu kingine; wamekamilika!


Hawataki hata Neno la Mungu kwa sababu ni wakamilifu; miaka ya 1940 hadi 1965, alitokea mjumbe alitwae William Branham, ambaye alitumwa na Mungu akihubiri juu ya uvuguvugu wao lakini hawakumwelewa wala hawakutaka kumsikiliza. Wakasonga mbele kwa ukamilifu ulio machoni pao.


Lakini neno la Mungu linakuja kwenu leo tena kwa sababu Bwana awapenda naye hataki mpotee na kutapikwa. ISKILIZENI SAUTI YAKE LEO!


Hivyo neno la subira ya Mungu ni neno juu ya utakatifu. Neno hili ndio analolisubiri Bwana Mungu likae ndani ya watu, hata watu hawa wafikie ukamilifu wa neno hilo. Na kama asemavyo NENO LA SUBIRA YANGU; maana yake utakatifu unaanza na maarifa yaani ufunuo utokao kwa Mungu. Ndipo kwa nini anasema NASIMAMA MLANGONI (Mstari wa 20), amesimama akiwa na neno hilo la kuwakamilisha watu hawa kutoka uvuguvugu na kuwa wakamilifu/watakatifu. 


Hilo ndilo neno la Subira yake, maana hilo halitanena kama wanenavyo walimu, na wachungaji, na mitume, na manabii wenu, na mababa (mapapa), na mapadre na makardinali waliofanywa na wanadamu. Halitokani na vyuo vya kitheolojia ndio maana hawalijui.


MAWASILIANO:

+255755 251 999

MANABII WA UONGO, Mahali wanakotoka

MANABII, NA AINA ZA MANABII

UJUZI WA MEMA NA MABAYA NI NINI NA KWA NINI NI DHAMBI

UADUI KATI YA UZAO WA MWANAMKE NA UZAO WA NYOKA

SABABU ILIYOPELEKEA ULIMWENGU WA KWANZA KUANGAMIZWA

        CHANGIA KUPITIA

 

          NMB:       22510119402

          MOBILE: 255755 251 999

​​

             MASHIBE ELIAS NTINGINYA

Mawasiliano:

 

+255 755 251 999

Mbezi, Dar-es salaam

  • Facebook
  • Instagram
  • X
  • TikTok
bottom of page