top of page

Injili ya kuzimu ni hekima au elimu juu ya nguvu za giza zinavyotenda kazi. Jinsi wachawi wanavyologa, jinsi freemason wanavyodhuru na kila kitu kinachosadikiwa kutumiwa na ufalme wa giza.


Mafundisho haya hasa yameletwa na wahubiri wa mafundisho ya mali (Mathayo 6:240 kwa ajili ya kutoa majibu juu ya uchumi wa watu. Ni kweli shetani yupo na mapepo na nguvu za giza za kila namna, lakini Bwana Mungu hakuagiza tuzijue sana nguvu za giza ili mtu apate amani bali amjue Mungu.


Basi, ikiwa nguvu za giza zipo ni kosa kuzijua?


Jibu ni hapana, lakini kuigeuza ibada ya kumjua Mungu iwe ya kumjua shetani ndio kosa. Lakini pia asili ya kila kitu ni Mungu, hivyo nguvu za giza zimekuwepo kwa sababu ya Mungu. Nazo zimekuwepo kama miiba kwa watendao maovu.


Hivyo injili inapaswa kumjua Mungu na kujitenga na uovu ili kuepuka kupokea mshahara wa mabaya. Lakini injili ya Laodikia apendaye mali anafundisha kuwa umasikini na matatizo yote yametokana na shetani, hivyo anajishughulisha kumjua shetani vizuri ili apate kujikinga na nguvu zake. Lakini nguvu za shetani zimekuwepo kwa sababu ya zile dhambi.


Imeandikwa;


33 Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.

Mathayo 6


Lakini Laodikia hataki kuketi barazani pa Mungu apate kumjua Mungu na kuoshwa dhambi zake zote, bali alipokwisha kukaribishwa katika ufalme wake akaingia na kuanza kutafta chakula na mavazi na magari apate kuwa tajiri na dhambi zake.


Ndipo wanapomwomba Mungu hukaa mbali na maombi yao. Na kwa sababu ni mafundisho batili, hawapati majibu sawasawa na maombi/mafundisho yao kutoka kwa Mungu. Ndipo kwa ujuzi wao hugeuka na kutafta wemyewe majibu hayo.


Ndipo utasikia umeibiwa nyota, una maagano ya ukoo, wamekunenea kushindwa, umeibiwa nyayo, walikutamkia umasikini ndio maana upo hivi leo, hawataki ufanikiwe kwa sababu una nyota kali sana, n.k. Haya si mafundisho ya Kristo, yametungwa kwa ueledi wa hao watamanio fedha.


Wakiisha kukufundisha hivi, wao ndio wamekuwa wamekuloga, na utaenda kutafta dawa ya kupona mikononi mwao.

Dawa ya kurudisha nyota, dawa ya kurudisha nyayo, dawa ya kufanikiwa, dawa mvuto wa mapenzi na biashara n.k.


Na kwa sababu injili yao ni ya kutunga, wala haitokani na Mungu, dawa yao mara nyingi huiuza kwa kila mtu awaendeaye. Hawatoi bure kwa sababu hawakupewa, bali waliitengeneza kwa jasho na bidii yao, Ubunifu huo ni kwao, huwezi kuwahukumu wala Mungu kuwahukumu kuwa wanamwibia kwa lile neno kuwa mmepewa bure toeni bure! 


Maana hawakupewa na Mungu bali wameitwaa kwa mwingine.

Pia hawawezi kutoa bure kwa sababu wanachokitafta kwako ni pesa yako, wala si kingine, hawakubuni mafundisho hayo isipokuwa kwa tamaa ya mali. Yeye anayewaendea walimu hawa ili apate mali, huishia kuwapa wao mali. 


Ukiondoa tamaa ya mali, mafundisho hayo yanaharibika na kuonekana kama kinyesi. Lakini walio na tamaa ya mali, mafundisho haya huwa kama maji katika nchi ya jangwa.


Mafundisho haya huenda mbali hata kuwanena wadudu kama mijusi na hata miti fulani kuwa ina mikosi. Kwa kuwa akili za watu hawa zimekwisha kulogwa na kwa tamaa yao mbaya, huishambulia miti hii na mijusi na nyoka kuwa wanaleta mikosi na kutokufanikiwa kwao.


Ndipo utaona walokole hawa wanamwogopa shetni na kuwa na wasiwasi na mashaka karibu kila kitu kinachowazunguka, na mara nyingi huwachukia mpaka majirani zao kwa kuwahisi wamewaibia nyota au kuwatakia mabaya waliyonayo. 


Wengine wameenda mbali kuelezea aina za mapepo au majini na nguvu zao na namna yanavyodhuru; utasikia pepo fulani linapendelea kukaa mahali fulani, pepo fulani linapendelea mavazi fulani ukivaa linakuingia.


Hii ni injili ya kutunga ambayo inapanda hofu ndani ya watu na kumwogopa shetani kuliko Mungu. Kila mtu anayetii mafudisho haya ajue na kufahamu kuwa amemwacha Kristo.


Imeandikwa;


Mathayo 10


²⁸ Msiwaogope wauuao mwili, wasiweze kuiua na roho; afadhali mwogopeni yule awezaye kuangamiza mwili na roho pia katika jehanum.

Kanisa linapoteza muda mwingi kuzungumzia habari ambazo si za ufalme wa Mungu, na watu wake wanamwogopa shetani kuliko Mungu.


Walimu hawa wanaofundisha mafundisho ya mali ndio hasa walimu wa mafundisho haya pamoja na walimu wa mafundisho ya awali ya Kristo, maana pia wangali watoto. Ndio maana mafundisho haya utayakuta kila dhehebu.


Neno la Mungu linasema laana na baraka zatoka kwa Mungu (Kumb 28). Aletaye laana na mikosi ni Bwana, sio wachawi wala mizimu wala miti wala mijusi.


Kama kuna kuibiwa nyota basi ni Mungu ndiye aliyetenda hivi, kama kuna laana ya ukoo, basi Mungu ndiye aliyetenda hivyo. Ni nani awezaye kupokonya mikononi mwake? Akamwamrisha achia na akaachia? Akapafungua alipopafunga au kupafunga alipopafungua? 


Ikiwa mnatafta nyota zenu, na utajili wenu, na baraka zenu ziizoibiwa kwa shetani, kwa nini kumwendea Mungu? ingefaa kuwaendee waganga na walozi walio watumishi wa shetani wawape nyota zenu.  Maana yeye huwapa walio wake kama ilivyoandikwa katika Mathayo 4:8-9. Lakini mtu anayemwendea Bwana kwa neno la uongo kutoka kwa walimu wake kuwa ameibiwa nyota, atapokea? 


Sikiliza Bwana asemavyo juu ya watu hao waulizao kwa Bwana majibu ya mafundisho waliojitungia, mafundisho ya mashetani;


Ezekieli 14,


4 Basi sema nao, uwaambie, Bwana MUNGU asema hivi; Kila mtu wa nyumba ya Israeli atwaaye vinyago  vyake na kuvitia moyoni mwake, na kuliweka kwazo la uovu wake mbele ya uso wake, na kumwendea  nabii; mimi, Bwana, nitamjibu neno lake sawasawa na wingi wa sanamu zake;

Ukimwendea Mungu kuuliza habari za utajiri, kuibiwa nyota, kufanikiwa katika biashara n.k hatakunyamazia, atakujibu sawasawa na sanamu zako, sawa sawa na mafundisho hayo ya mashetani, sawa sawa na tamaa yako ya mali. Ndipo utaona mara umeoneshwa mizimu ya ukoo na maagano waliyoweka ukiwa mtoto au upo tumboni au mtu mzima, utaona vita vya wachawi juu yako n.k.  Yeye Bwana anakudanganya kwa sababu unaabudu uongo.


9 Na nabii akidanganyika, na kusema neno, mimi, Bwana, nimemdanganya nabii yule, nami nitaunyosha  mkono wangu juu yake, na kumwangamiza, asiwe kati ya watu wangu Israeli.

Ezekieli 14


Ndivyo Bwana anavyowadanganya watumi wenu wamwendeaye kumuuliza kwa habari ya mafundisho yao waliojitungia, na tamaa zao na ulozi wao na ushirikin wao. Bwana huwadanganya walimu, wachungaji, na mapadre, na manabii, na mitume, na maasikofu na kila viongozi wenu walioweka sanamu (mafundisho ya uongo) katika paji zao za uso.

  

Ndipo Laodikia ajionapo tajiri kwa mafundisho yatokanayo na uongo wa Bwana. Na kwa sababu Bwana amewadanganya, majibu muyapatayo, si kweli na hayawezi kuwa. Ndio kila unabii akuambiao nabii wako hautimii, amani aliyokutabiria haiji wala neno lolote la baraka kuto kwao halitimii. 


Na kwa sababu hii, ndipo maombi ya KUSHINDANA/KUKEMEA ya walokole yamepewa nafasi ya kwanza lakini ndio maombi ya yasiyo maana. Ni maombi ya damu na nyama kulazimisha iwe, sawasawa na mafundisho yao ya uongo. 


Sikiliza sauti ya Bwana, shetani hamlaani mtu, isipokuwa anaweza kumdhuru aliyelaaniwa na Mungu. Maana laani ni kuondolewa kwa ulinzi wa Mungu, ndipo shetani hupata njia.

.

Basi kila aliyetumwa na Mungu huwafundisha watu kulitii neno lake liondoalo dhambi, na kumwogopa Mungu. Lakini mwalimu mpumbavu, huigeuza injili ya Bwana, na kuwaambia watendao uovu kuwa ogopeni umasikini, ogopeni njaa, ogopeni wachawi waibao nyota zenu, ogopeni paka weusi, njoo mkanyage mafuta na maji na chumvi muondoe laana na mikosi! 


Hivi ndivyo wawaambiavyo, na hofu yenu kwa Mungu ni haya mafundisho ya wanadamu yaani uongo. Na huo ndio uvuguvugu, Laodikia anao upenda.  Mwasemaje? Je, Mungu atayanyamazia haya, Yeye atafurahishwa na udhalimu? Atabadilika moyo kwa ajili ya tamaa zenu? Au mtaubadilidha moyo wake kwa kuwa ninyi ni wengi?


Hapana, mkono wake umeinuka juu yenu hata sasa ili kujipatia utukufu. Ninyi ndio mtaleta sifa na ukuu kwake siku hii ya ghadhabu yake. Kama wale watu walivyokataa kumsikia nuhu, gharika ile hata leo huhubiriwa. Bwana alijizoelea utukufu kwa sababu ya mioyo migumu ya watu wale, na Kristo mnayesema tunampenda alisema jambo hilo hilo kutokea nyakati hizi.


Na kama ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo itakavyokuwa katika siku zake Mwana wa Adamu.

Luka 17:26.


Naam, ISIKILIZENI SAUTI YA BWANA.


Mawasiliano;

+255755251999.

MANABII WA UONGO, Mahali wanakotoka

MANABII, NA AINA ZA MANABII

UJUZI WA MEMA NA MABAYA NI NINI NA KWA NINI NI DHAMBI

UADUI KATI YA UZAO WA MWANAMKE NA UZAO WA NYOKA

SABABU ILIYOPELEKEA ULIMWENGU WA KWANZA KUANGAMIZWA

        CHANGIA KUPITIA

 

          NMB:       22510119402

          MOBILE: 255755 251 999

​​

             MASHIBE ELIAS NTINGINYA

Mawasiliano:

 

+255 755 251 999

Mbezi, Dar-es salaam

  • Facebook
  • Instagram
  • X
  • TikTok
bottom of page