top of page

Juzi siku ya tarehe 12/8/2026, kulionekana ishara ambayo tunaijua kama kupatwa kwa jua, yaani mwezi kuwa kati ya dunia na jua. Mwezi ukiwa kati ya jua na dunia, unazuia mwanga wa jua kufika duniani. Hivyo sehemu ya dunia inakosa mwanga.


Kitendo hiki ni sehemu ya matukio ya asili, ambayo huwezi kuyazuia wala kupanga yatatokea lini, bali unaweza kujua wakati gani yatatokea. Lakini ni tukio linahubiri injili ya Mungu wakati wote kwa kila aliye katika ulimwengu huu.


Siku zote mwezi unawakilisha kanisa, jua linawakilisha Mungu au Neno litokalo kwa Mungu kwa njia ya nabii. Dunia ni mahali anapoishi mwandamu. Hivyo, mwezi kuwa katikati ya jua na dunia maana yake ni Kanisa kuwa kati kati ya Mungu na dunia.


Kwa sababu hiyo kanisa linazuia nuru ya Mungu isiufikie ulimwengu na kufanya giza katika ulimwengu. 


MAANA YAKE NINI?


Unafahamu kuwa kanisa ni watu wanoongozwa na Mungu, na ya kuwa ndiyo mpatanishi kati ya watu wa ulimwengu na Mungu, hilo ni kweli, lakini kanisa hilo hilo huwa kikwazo na kuwazuia watu wasipate kumsikiliza Mungu.


Nuru ya Mungu yaani neno lake, linapokuja kwa ulimwengu huja kwa njia ya manabii, kwa jina lingine malaika, kama Musa, Isaya, Yeremia, Yesu Kristo, n.k. Nuru yao ndio Nuru ya Mungu kwa sababu wameipokea kutoka kwa Mungu wapate kuingaza kwa ulimwengu.


Lakini kila wakati Bwana Mungu anapolituma neno hilo hukutana na kipingamizi cha kanisa. Hilo kanisa ni watu waliopokea nuru iliyokuwako, lakini shetani akaitia giza ile nuru kwa mafundisho ya uongo na tafsiri za damu na nyama, yaani wanadamu. Kwa sababu hiyo badala ya kanisa kutoa nuru kwa ulimwengu, wanatoa giza.


Lakini lile giza ni nuru kwao, ndio injili kwao. Nuru hizo ni hayo madhehebu,  Isaya anaziita nuru hizo kuwa ni taa au mienge walijiwashia watu hao na kuwafanya kuikataa nuru halisi ya Mungu.


11 Tazama, ninyi nyote mwashao moto, mjifungiao hiyo mienge; endeni ninyi katika mwali wa moto wenu, na katikati ya mienge mliyoiwasha. Mtayapata haya kwa mkono wangu; mtalala kwa huzuni. 

Isaya 50:11


Hapa Isaya alikuwa akizungumza na madhehebu ya kiyahudi katika kipindi chake, waliompinga na kukataa kutubu ili wautumikie uongo. Vile vile Yesu Kristo alikutana na kuzuizi kama hicho cha kanisa alilolikuta na hata manabii wengine nao vile vile.


Kwa nini ni kanisa ndio limekuwa kinyume na Mungu na si watu wa ulimwengu? Kizazi hata kizazi ni kanisa ndio humpinga Mungu, na kuipuuza nuru yake kuwa ni uongo, ili wazifanye nuru zao zisizime. Sababu ni kuwa kanisa linakwenda kwa ufunuo wa damu na nyama na si ufunuo wa Mungu.


Na ufunuo wa damu na nyama hutokana na shetani, ndipo kanisa huibadili kweli kuendana na baba wa huo ufunuo, yaani shetani. Naam, kutokana na siri ya ufunuo iliyopo, kanisa linabaki likiamini ufunuo huo umetoka kwa Mungu na kwa sababu hiyo linamtumikia shetani badala ya Mungu kwa kutokujua.


Kisha neno la Mungu likija kwao hulipinga kwa sababu linaenda kinyume na roho ya mafundisho yao. Haku ndiko mwezi kuzuia nuru ya jua isifike ulimwenguni, ili ulimwengu ubaki gizani yaani katika mienge waliojiwashia.


Hivyo lile giza liletwalo na mwezi wakati ukiwa katikati ya dunia na jua ni mafundisho ya uongo ya madhehebu, ambayo huwa nuru kwa watu waliopo ndani ya kanisa isipokuwa siku za neno la Mungu. 


Katika siku za kuja kwake kwa neno la Mungu kama hivi leo, zile nuru za madhehebu (kanisa) hugeuaka kuwa giza kwa ulimwengu. Nazo husimama kama kikwazo cha watu dhidi ya neno la Mungu ili watu wasipate kuijua nuru halisi hata wapate kutubu.


Je, hata sasa mngali hamjui bado? Itakafarini siku hii leo kabla Bwana hajaugeuza mwezi kuwa damu, enyi watu wa shingo ngumu. Vizazi hata vizazi wanadamu hawajawahi kupata kujua dhambi yao, hata wanapoitwa kutubu hupingana na Mungu kuwa wao hawana dhambi.


Laodikia, ISIKILIZE SAUTI YA BWANA, MUNGU WAKO, usiangamie bali upate kuishi. Maana hata wewe hutaki kutubu ukisema huna haja na kutubu, ukipinga neno la Mungu kwa utajiri wa uongo ulijitajirisha, ufunuo wa damu na nyama.


¹⁴ Na kwa malaika wa kanisa lililoko Laodikia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye Amina, Shahidi aliye mwaminifu na wa kweli, mwanzo wa kuumba kwa Mungu.
¹⁵ Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto.
¹⁶ Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu.
¹⁷ Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, NIMEJITAJIRISHA, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi.

Ufunuo wa Yohana 3


Laodikia, wewe ni mwezi uliopaswa kuangaza nuru ulimwenguni kwa kuakisi nuru ya Mungu (ufunuo wa Mungu). Nuru yako aliyokupa Bwana umeichanganya na nuru isiyotoka kwa Mungu (giza), na nuru yote imekuwa giza , naye Bwana amekuijilia lakini huitaki nuru yake. Kwa nini uwe mazomeo wewe nawe kama alivyokuwa Israeli?


Mawasiliano;

(+255) 0755 251 999

SIKU YA SABATO NI IPI?

SABATO NI NINI?

KUPATWA KWA JUA KUNAMAANISHA NINI KATIKA ROHO?

MATENDO YA SHERIA NI NINI NA KWA NINI HAYALETI HAKI?

NEEMA, NA MAUTI ILETWAYO NA NEEMA!

        CHANGIA KUPITIA

 

          NMB:       22510119402

          MOBILE: 255755 251 999

​​

             MASHIBE ELIAS NTINGINYA

Testaments :

+255 755 251 999

Mbezi, Dar es Salaam

  • Facebook
  • Instagram
  • X
  • TikTok
bottom of page