top of page

Uzao wa nyoka umetajwa mara kadhaa katika maandiko matakatifu, Bwana Yesu na Yohana mbatizaji walitumia maneno hayo wakati wa kuhubiri kwao. 


Yohana mbatizaji;


7 Hata alipoona wengi miongoni mwa Mafarisayo na Masadukayo wakiujia ubatizo wake, aliwaambia, Enyi wazao wa nyoka, ni nani aliyewaonya ninyi kuikimbia hasira itakayokuja? 

Mathayo 3:7




Yesu Kristo;


33 Enyi nyoka, wana wa majoka, mtaikimbiaje hukumu ya jehanum?

Mathayo 23:33


34 Enyi wazao wa nyoka, mwawezaje kunena mema, mkiwa wabaya? Maana, kinywa cha mtu huyanena yaujazayo moyo wake. 

Mathayo 12:34


Hizo ni sehemu unaweza kupata maneno hayo, Swali ni kwamba kwa nini walitumia maneno haya? Walikuwa na hasira wakawatukana wale watu? Maana nyoka tunamjua, hazai mwanadamu.


Ndio zilikuwa ni hasira, lakini hayakuwa matusi, ila ni ukweli uliofikishwa kwa njia ya moja kwa moja, maneno kama haya hutamkwa kwa sababu ya ghadhabu ya Mungu, mara nyingi huwafanya walengwa wakasirike badala ya kujifunza makosa yao na kutubu lakini ndivyo yalivyokusudiwa, kwamba wasitubu kwa sababu ya shingo zao ngumu.


Kwa upande wao walihesabu kuwa ni matusi na hata mtu mwingine pia anaweza kuhesabu yale kuwa ni matusi. Lakini matusi huwa hayana ukweli ndani yake isipokuwa kusingizia au kudhalilisha na mambo kama hayo. Twende tukautazame uzao wa nyoka upate kujua kwa nini wallitwa uzao wa nyoka.


1 Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya Bwana Mungu. Akamwambia mwanamke, Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile matunda ya miti yote ya bustani? 
2 Mwanamke akamwambia nyoka, Matunda ya miti ya bustanini twaweza kula; 
3 lakini matunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu amesema, Msiyale wala msiyaguse, msije mkafa.
4 Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa, 
5 kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya. 

Mwanzo 3:1-5


Bwana alimwagiza Adamu matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, ukila utakufa hakika (Mwanzo 2:16-17). Lakini hapa Nyoka akaja kwao kwa injili ya uongo, akalipindua neno la Mungu kwa weledi wa ajabu. Adamu na Hawa wakala yake matunda aliyokataa Bwana Mungu kwa kumwamini Nyoka.


Injili kama hiyo ipo mpaka leo hii, inabadilika majina tu, katika Israeli ilichukua jina la mafundisho ya Balaam au Yezebeli na katika agano jipya inachukua jina la mafudisho Wanikolai.


Chimbuko la uongo lilianzia hapa kwa Nyoka, akamdanganya Hawa, naye Adamu akala kwa ushawishi wa mkewe. Maana yake walikubaliana na nyoka kuwa hawatakufa na ya kwamba watafanana na Mungu. Injili hii ndio iliyobaki mioyoni mwao tangu wakati huo badala ya ile ya Mungu.


Injili ya nyoka huja kila wakati Neno la Mungu linapokuja, ilikuja ilikuja baada ya Torati ya Musa, zikaingizwa tafsiri za uongo nyingi hata kufanya ule uongo kuwa ndio neno la Mungu. Kwa sababu ule uongo ndio uliishi mioyo mwa watu na kuliondoa ile kweli ya Mungu. 


8 Mwasemaje, Sisi tuna akili, na torati ya Bwana tunayo pamoja nasi? Lakini, tazama, kalamu yenye uongo ya waandishi imeifanya kuwa uongo. 

Yeremia 8:8.


Yeremia wakati anahubiria watu hawa watubu, walijiona hawana kosa. Wanayo torati ya Musa na wanaenda kama torati isemavyo, lakini Yeremia anawaambia kalamu ya uongo imeifanya torati kuwa uongo. Kalamu ya uongo ni tafsiri zinazotoka kwa walimu, wachungaji, maaskofu, mapadre n.k, tafsiri kama zile za nyoka. Tafsiri za uongo zinazogeuza neno la Mungu lionekane uongo.


Kwa sababu hiyo watu waliozaliwa kwa mafundisho ya namna hiyo ni uzao wa Nyoka. Hivyo Yohana pamoja na Yesu walikuwa wanatumia uzao wa nyoka kumaanisha wale wa madhehebu wamezaliwa katika mafundisho ya uongo, mafundisho ya nyoka. Nao wameshika uongo kama mtu ashikavyo kweli, naam, uongo ndio hofu yao mbele za Mungu. Ibada kama hizo ni sanamu mbele za Mungu!


Watu wa namna hii hawawezi Huwezi kubadilika kirahisi hata kama utasimulia sana. Maana kwao kuacha mafundisho hayo ni kama kumwacha Mungu. Isaya alitabiri juu yao akisema;


“Ni nani aliyesadiki habari tuliyoileta? Na mkono wa Bwana amefunuliwa nani?”

 Isaya 53:1 (Biblia Takatifu)


Ndipo kwa nini Kristo alitumia ishara na miujiza kwavuta wenye mioyo ilipondeka, lakini waliojiona wana torati, hakutaka hata wajue Yeye ni nani, akanena kwa mifano wasije wakaelewa wakatubu akawaponya.


Mathayo 13 (Biblia Takatifu)


¹⁰ Wakaja wanafunzi, wakamwambia, Kwa nini wasema nao kwa mifano?
¹¹ Akajibu, akawaambia, Ninyi mmejaliwa kuzijua siri za ufalme wa mbinguni, bali wao hawakujaliwa.
¹² Kwa maana ye yote mwenye kitu atapewa, naye atazidishiwa tele; lakini ye yote asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyang'anywa.
¹³ Kwa sababu hii nasema nao kwa mifano; kwa kuwa wakitazama hawaoni, na wakisikia hawasikii, wala kuelewa.
¹⁴ Na neno la nabii Isaya linatimia kwao, likisema, Kusikia mtasikia, wala hamtaelewa; Kutazama mtatazama, wala hamtaona.
¹⁵ Maana mioyo ya watu hawa imekuwa mizito, Na kwa masikio yao hawasikii vema, Na macho yao wameyafumba; Wasije wakaona kwa macho yao, Wakasikia kwa masikio yao, Wakaelewa kwa mioyo yao, Wakaongoka, nikawaponya.

Hivyo ni wazi alitumia mifano kwa sababu hakutaka kuwaponya. 


Lakini ni wakina nani hao waliokuwa na hayo mafundisho ya nyoka walio uzao wa nyoka?


Zilikuwepo injili aina mbali mbali yaani madhehebu, kama Wafarisayo, wasadukayo, wazelote, waesene (waesenayo), n.k. Haya madhehebu yote ndio uzao wa nyoka. Maana injili zao zimejaa tafsiri za uongo na kufanya mafundisho yao yawe ya uongo.


Naam, mafundisho ya nyoka yapo kila dhehebu leo unaloliona na unalolisikia. Yalikuwepo katika kizazi cha Nuhu, yalikuwepo katika kizazi cha Yakobo, na Yapo katika kizazi cha Yesu Kristo hata leo.


Ndio maana kuja kwake mara ya pili alisema itakuwa kama siku za Nuhu, na hapa ningeweza kusema itakuwa kama siku za kuja kwake mara ya kwanza, lakini isipokuwa hakutakuwa na miujiza kama mara ya kwanza lakini kizazi ni kile kile cha nyoka.


Nadhani kwa kusikia hivyo umekasilika, lakini hiyo haibadili hatima yako. Kitakachobadili hatima yako ni kuipenda kweli na kutubu.


NYOKA ALIZINI NA HAWA?


Ipo dhana au mafundisho yanayofundisha uzao wa nyoka kwa namna ya kinwili, kwamba Nyoka alilala na Hawa ndipo akazaliwa kaini, lakini Habili akatoka kwa Adamu. Na kwa sababu hiyo hunenwa Kaini na wote wanaotenda dhambi ni kwa sababu walizaliwa na Nyoka. Hiyo si kweli, Hakuna mwanadamu aliyezaliwa na Nyoka kimwili. 


Isipokuwa yule apendaye injili ya nyoka, hubatizwa katika na kuzaliwa mara ya pili katika hiyo. Mtu anakuwa mtoto wa Mungu kwa sababu anatubu na kuliamini neno lake, lakini uongo ujapo akauamini, Baba yake anatoka kuwa Mungu na kuwa wa Nyoka.


ISIKIKIZENI SAUTI YA BWANA.


Mawasiliano:


+255 755 251 999

MATENDO YA SHERIA NI NINI NA KWA NINI HAYALETI HAKI?

NEEMA, NA MAUTI ILETWAYO NA NEEMA!

ANDIKO HUUA BALI ROHO HUHUISHA

WASIO HAKI HUNENAJE KWA LUGHA?

HAKUTAKUWA NA UNYAKUO JUU YA KIZAZI HIKI!

        CHANGIA KUPITIA

 

          NMB:       22510119402

          MOBILE: 255755 251 999

​​

             MASHIBE ELIAS NTINGINYA

Wills:

+255 755 251 999

Mbezi, Dar es Salaam

  • Facebook
  • Instagram
  • X
  • TikTok
bottom of page