top of page
6 Naye ndiye aliyetutosheleza kuwa wahudumu wa agano jipya; si wa andiko, bali wa roho; KWA MAANA ANDIKO HUUA, BALI ROHO HUHUISHA.

2 Wakorintho 3


Andiko ni kile kilichoandikwa baada ya kunenwa na Mungu kwa njia ya manabii. Neno hilo huwa limefichwa katika mafumbo ili walio haki wapate nuru na waovu watiwe giza kwa neno hilo hilo.


Kama hekima ya ulimwengu huu isemavyo, fumbo mfumbie mjinga, mwerevu atalitegua. Ndivyo na katika ufalme wa mbinguni, walio haki watapewa kujua mafumbo hayo, lakini wasio haki watatwaa maana nyingine iliyo sawa na uovu wao.


Tafsiri ya lile andiko ikiwa ni ya uongo huleta mauti kwa maana huwafanya wasio haki waseme uongo, lakini Roho huileta tafsri ya kweli kwa njia ya malaika zake ili kuhuisha yaani kuondoa ule uongo, na walio haki huisikia sauti yao.


Tazama mfano wa andiko hili kwa Adamu,


16 Bwana Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema, Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula, 

17 walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika.

Mwanzo 2:16-17.


Hapa, neno la Mungu, ambalo lilikuwa ni andiko lenye fumbo. Adamu na Hawa walijiuliza kuna ubaya gani katika ujuzi wa mema na mabaya. Kwa nini tufe kwa kupata ujuzi wa mema na mabaya. Mungu alimaanisha nini hasa?


Ndipo Nyoka akaja na tafsiri ya hilo andiko, akisema;


4 Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa, 
5 kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya. 
6 Mwanamke alipoona ya kuwa ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa, basi alitwaa katika matunda yake akala, akampa na mumewe, naye akala.

Mwanzo 3:4-6.


Hii ni tafsiri ya mwalimu asiye haki, akitafsiri alichokisema Bwana Mungu. Tafsri hii ilikuwa inaleta mantiki, Hawa hakuwa mjinga kukubali kirahisi, ni tafsiri ilikuwa na mashiko, kweli yenye uongo. Nyoka alipunguza na kuongeza yaliyo yake mwenyewe. Walipokula tunda hili ndipo wakajua tumedanganyika.


Tazama pia andiko moja linalohusu neema, ambayo ni upendo wa Kristo. Wako watu wanaoitafsiri neema kwa namna hiyo hiyo, lakini upendo huo wameugeuza uwaelekee wao, uwe upendo unaoendana na matakwa yao.


Ndipo utasikia mashoga wahubiri, wazinzi wahubiri, washirikina wahubiri, na kila aina ya uhuni utauona umesimama mahali patakatifu wakihubiri upendo wa Kristo. Tafsiri yao ni kuwa upendo wa Kristo haufungwi na dhambi, upendo wa Kristo ni mkubwa kuliko tunavyodhani. Hakuna kinachotutenga na upendo wa Kristo, hakuna mwanadamu wa kututenga nao.


Na kwamba kwa kuwa wangali wakimpenda Kristo, Kristo anaangalia mioyo yao na upendo wao. Watu hawa huitafsiri neema ya Kristo kama nyoka alivyotafsiri, ni watu wa baba mmoja, kupitia andiko wanakula kisicho haki.


Kristo alisema mkinipenda mtazipenda amri zangu, upendo mwingine tofauti na huo unatoka kwa ibilisi. Lakini wangali watasema amri zake ni kumpeda kwa moyo wetu wote na jirani yetu kama nafsi yetu. 


Naam, sheria ni hizo zilizo kuu, na kwa sababu hiyo muovu kwa kuzipenda amri hizo kama zilivyoandikwa amekalia kiti cha walio hai. Ndivyo lilivyo andiko, lakini Roho yake sio hayo maneno bali maana yake. Kumpenda Mungu ni kujitenga na uovu, si kutenda ule uovu. Na kupenda jirani ni kumsaidia kama kuifanyia nafsi yako mwenyewe si kwa kuongea kwamba unampenda.


13 Kumcha Bwana ni kuchukia uovu; Kiburi na majivuno, na njia mbovu, Na kinywa cha ukaidi pia nakichukia.

Mithali 8


Lakini upendo wa watu hawa ni kupenda maovu, huku vinywa vyao wameviweka mbinguni kuwa Mungu anawapenda na wao wanampenda.


Andiko halipotoshi wala kudanganya hata lilete mauti, bali asomaye ndiye hulipotosha na kusema uongo juu yake. Na hekima nyingi zilizopo ulimwenguni kwa sasa, kwa maana ya theolojia, ni tafsiri za maandiko pasipo Roho wa Mungu, bali zimekuwepo kwa sababu ya ufunuo wa damu na nyama.


Lakini kila mmoja alichokipata katika kutafsiri kwake yaani kila theolojia ni sahihi na imevuviwa na Roho mtakatifu machoni pa mtu huyo, hata imekuwa kwamba hamna aliyekosea isipokuwa asiye wa theolojia hiyo. Tazama andiko hili;


18 Namshuhudia kila mtu ayasikiaye maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mtu ye yote akiyaongeza, Mungu atamwongezea hayo mapigo yaliyoandikwa katika kitabu hiki. 
19 Na mtu ye yote akiondoa lo lote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima, na katika ule mji mtakatifu, ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki.

Ufunuo wa Yohana 22:18-19


Haya ni maandiko, na utayakuta kila dhehebu, lakini kila dhehebu huyatafsiri kama yalivyo kwamba hawajaongeza wala kupunguza, isipokuwa wengine wasio wa theolojia yao. Na kwa sababu hiyo kila dhehebu hujiona hawana hatia. 


Lakini kimsingi kila mmoja ameongeza na kupunguza. Kisha andiko hili hulitumia kuwapa uzima na kujihesabia haki kuwa theolojia yao ndio kweli. Na kila anayetaka kuhoji hiyo kweli yao (theolojia yao), huyasoma maandiko hayo hayo kuwa ndio muongozo wa yeye kuelewa theolojia yao.


Katika Israeli na vizazi vilivyopita vilikuwa katika namna hiyo hiyo, hata kwamba watu huishi mautini kwa sababu ya lile andiko. Na Roho wa Mungu anawaijiriwa watu hawa ndipo wao humwona akiongeza na kupunguza katika neno la Mungu. 


Humhukumu kwa kumlinganisha na theolojia zao ambazo hazijaongezwa wala kupunguzwa kwa mjibu wa andiko. Ndipo andiko hilo hilo ambalo huzani wanao uhai ndani yake na wakati ndio linalomshuhudia Yule Roho mtakatifu kuwa amekuja kuwahuisha, wanalitumia kuwalinda na Roho mtakatifu wasitoke katika uongo wao. Naam, ndivyo ilivyo kwa kizazi hiki pia.


Israeli alimwona Roho wa Mungu aliyekuja kuwahuisha kutoka mauti kwa sababu ya andiko kuwa anamkufuru Mungu kwa kujiita Mwana wa Mungu. Kwa kutumia andiko walijua Mungu amesema hakuna Mungu isipokuwa yeye, ametajwa kuwa ni mmoja, hazai, hana mke. (Kumb 6:4, Isaya 44:6 n.k).


Lakini walisahau kuwa Bwana katika kitabu chao cha Mwanzo alisema Wana wa Mungu walioa binti za wanadamu! Hawakuichana kurasa hii kwa sababu inamkufuru Mungu asiye zaa. Naam, walikuwa na andiko hawakuwa na Roho. Naye Roho alipokuja kwao wakamkataa kwa ajili ya andiko.


Ndivyo kilivyo kizazi hiki hata leo. Maandiko yapo, ndio Biblia, lakini kalamu za uongo za waandishi ni nyingi, nazo zinanena kila moja andiko linasema, andiko linasema! Ni kweli andiko linasema, lakini tafsiri ni ya wanadamu.


ISIKILIZENI SAUTI YA BWANA!


Mawasiliano;


(+255) 0755 251 999.

MATENDO YA SHERIA NI NINI NA KWA NINI HAYALETI HAKI?

NEEMA, NA MAUTI ILETWAYO NA NEEMA!

ANDIKO HUUA BALI ROHO HUHUISHA

WASIO HAKI HUNENAJE KWA LUGHA?

HAKUTAKUWA NA UNYAKUO JUU YA KIZAZI HIKI!

        CHANGIA KUPITIA

 

          NMB:       22510119402

          MOBILE: 255755 251 999

​​

             MASHIBE ELIAS NTINGINYA

Wills:

+255 755 251 999

Mbezi, Dar es Salaam

  • Facebook
  • Instagram
  • X
  • TikTok
bottom of page