top of page

Neema ni zawadi, fadhili, wema au kibali anachopokea mtu bure pasipo yeye mwenyewe kustahili kwa matendo yake. Injili ya Yesu Kristo pia inaitwa injili ya neema kutokana na neema aliyoitoa Yesu Kristo.


Yesu Kristo alikufa msalabani kwa makosa au dhambi isiyo yake, bali ya watu walio katika ulimwengu. Badala ya wenye dhambi kufa kwa ajili ya dhambi zao, yeye alijiweka nafsi yake badala ya nafsi zao.


Kisha ile mauti aliyokufa inahesabiwa kuwa ni mauti waliokufa wenye dhambi waliokubali kuipokea hiyo zawadi (mauti ya Kristo), kwa ishara ya kuzamishwa katika maji.


Kifo cha Kristo ndio neema au zawadi aliyoitoa ili kuwafanya wengi waliokuwa wanahesabiwa kuwa ni wa mautini kwa ile dhambi yao kuwa hai. Hakuna mtu aliyemlipa Kristo fedha kufanya  hivyo, wala si kwa sababu ya haki yetu hata akafa, wala hakuna aliyekuwa anamdai, hata aseme alikuja kunilipa deni langu kwa kufa badala yangu. 


Bali aliupenda tu ulimwengu uokolewe kutoka katika mauti ya milele. Na huo ndio upendo wa Mungu ulio mkuu, kuutoa uhai wake kwa ajili ya wengine.  Kwa maneno mengine neema ni UPENDO WA MUNGU.


Mambo haya ni mafundisho ya awali ya Kristo (maziwa) ambayo mmekuwa na walimu wengi wajuao kuelezea mambo hayo tangu Paulo.


Lakini nataka ujue neema haijakuwapo wakati wa Kristo tu, hapana, imekuwepo tangu mwanzo. Ijapokuwa neema hizo hazikuwa kubwa kama hiyo iliyokuja kwa njia ya Yesu Kristo.


Neema utaiona wakati wa wana wa Yakobo (Israeli), wakitolewa kutoka katika mikono ya Misri mwana wa Hamu. BWANA MUNGU alituma mauti kwa kila mzao wa kwanza wa wana wa Misri, Yakobo hakunyanyua upanga juu ya Misri ili kupata uhuru. Lakini kazi yote ilifanywa na Mungu, na Israeli akamsifu Mungu siku hiyo kwa kumpa wokovu.


Tazama vizuri mwenendo wa  wana wa Israeli walipokombolewa kwa Neema ya Bwana kutoka katika nchi ya Misri. Walipovuka tu ile bahari ya sham, mambo yakaanza kubadilika.


Mungu akawageukia wao badala ya wana wa Misri mwana wa Ham. Hapo kwanza walimpenda Mungu na kumsifu kwa mkono wake aliounyosha juu ya adui zao. Wakaifurahia hiyo neema, wasitafakari yaliyomkuta misri yanaweza kuwakuta wao.


Neema ina mambo mawili,  kuangamiza na kuokoa. Wana wa Israeli walisahau kuwa neema ilikuja kwao kwa njia ya hukumu kwa wamisri. Wakati wao wanaokolewa, Misri anateketea kwa hasira ya Bwana. Lakini Israeli hakutafakari hayo, Yeye alijipaka usoni utukufu wa neema na upendo wa Mungu asioujua tabia yake.


Ndipo baada ya kitambo kidogo kutoka Misri Miriamu akiendelea kutunga nyimbo kumsifu Bwana kwa wokovu wake, Mkono wa Bwana ukaja juu yao pia, kiasi cha kutaka kuwaangamiza wote pia. 


7 Bwana akamwambia Musa, Haya! Shuka; kwa maana watu wako uliowatoa katika nchi ya Misri wamejiharibu nafsi zao, 
8 wamepotoka upesi kuiacha ile njia niliyowaamuru, wamejifanyizia ndama ya kuyeyusha wakaiabudu na kuitolea dhabihu, wakasema, Hiyo ndiyo miungu yako, Ee Israeli, iliyokutoa katika nchi ya Misri. 
9 Tena Bwana akamwambia Musa, Mimi nimewaona watu hawa, na tazama, ni watu wenye shingo ngumu

10 basi sasa niache, ili hasira zangu ziwake juu yao, niwaangamize, nami nitakufanya wewe uwe taifa kuu. 

Kutoka 32


Bwana Mungu hata asingekumbuka kuwa alipoteza muda kuwakomboa, asingejali sifa alizopata miongoni mwa watu hawa baada ya kuvuka bahari na wamisri wakaangamia ndani yake. Lakini kwa sababu ya Musa, Bwana Mungu alikumbuka rehema, akawapa torati. Wakaenda kanaani, lakini mioyo yao ikabaki Misri. 


Miaka mingi baadae akawaijilia kwa manabii baada ya upendo wao kupoa. Lakini wakati huo nao hawakumtambua kuwa ni Yeye aliyetupa ile neema tukatoka ile nchi ya uvuli wa mauti. Wakaitazama ile neema ya kwanza badala ya ya maneno yake yanayohubiriwa kwao wakati huo. 


Ndipo wakati wa Yesu Kristo ile neema yake ikaleta mauti kwao kama alivyotabiri Isaya;


4 bali kwa haki atawahukumu maskini, naye atawaonya wanyenyekevu wa dunia kwa adili; naye ataipiga dunia kwa fimbo ya kinywa chake, na kwa pumzi ya midomo yake ATAWAUA WABAYA.

 

Isaya 11:4


Wakati anatenda jambo hilo la kuwaua wabaya waliowazuri machoni pao, waliokuwa wakitumainia wema wa Mungu wa kwanza katika nchi ya misri kuwa ndivyo ulivyo siku zote, aliwaokoa walio isikia sauti yake na kuitii. Ambao ndio wakristo leo.


Lakini bado uko unabii juu ya hao washikao neema ambao nao wamibatilisha kwa kupanda uovu ndani yake.


17 Lakini iwapo matawi mengine yamekatwa, na wewe mzeituni mwitu ulipandikizwa kati yao, ukawa mshirika wa shina la mzeituni na unono wake, 

18 usijisifu juu ya matawi yale; au ikiwa wajisifu, si wewe ulichukuaye shina, bali ni shina likuchukualo wewe. 
19 Basi utasema, Matawi yale yalikatwa kusudi ili nipandikizwe mimi. 
20 Vema. Yalikatwa kwa kutokuamini kwao, na wewe wasimama kwa imani yako. Usijivune, bali uogope. 

21 Kwa maana ikiwa Mungu hakuyaachia matawi ya asili, wala hatakuachia wewe. 

Warumi 11:17-21.


Huu unabii juu ya watu wa neema, walioamini na kujivuna kwa kuamini kwao wakiwabeza wayahudi waliomsulubisha Yeye aliye ndiye kwao. Lakini iko ahadi kwa uzao huu nao kuwa wakati wa kuijiriwa Israeli, sharti wabaya wauawe katika hao waliomwamini.


Hiyo ndio siku ya kuja kwake, kuangamiza wabaya na kuokoa watakaoamini. Maana katika hao waliomwamini huihesabu neema ya kwanza kuwa ndio wokovu wao. Lakini hata sasa Kristo anasema kanisa ni vuguvugu Ufunuo 3:14-20.

Tena kwamba anasema nitakutapika kama hutatubu.
16 Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu.

Ufunuo wa Yohana 3:16


Ijapokuwa wengi hunena wakisema tunasubiri unyakuo, Neno la Kristo linasema wewe si moto wala si baridi. Maana kama Musa alivyotabiri kuwa atakuja nabii kama mimi, ISIKILIZENI SAUTI YAKE; 

18 Mimi nitawaondokeshea nabii miongoni mwa ndugu zao mfano wako wewe, nami nitatia maneno yangu kinywani mwake, naye atawaambia yote nitakayomwamuru. 
19 Hata itakuwa, mtu asiyesikiliza maneno yangu atakayosema yule kwa jina langu, nitalitaka kwake.

Kumbukumbu la Torati 18


Naam, ndivyo na katika kizazi hiki asemavyo ISIKILIZENI SAUTI YANGU, Kwa kuwa ni vuguvugu, si baridi wala moto. Na kila asiyeisikiliza sauti yake leo atatengwa na Kristo, maana amesema,  nitakutapika utoke katika kinywa changu. 


Hivyo ni hali ile ile ya kuijiriwa, aliyekuwepo anaangamia kwa kutokuamia kwake, na yule aliyeketi akingojea nuru ya Bwana atapona. Niseme nini juu ya kizazi hiki, ambacho kinaitazama neema kuliko neno lake na sauti yake? neema hiyo ndiyo imewafanya kuwa vipofu, hawaijui dhambi yao, hata wamejiweka tayari kuangamia.


Hivyo neema sio HAKI KAMILI baki mlango wa kuingia katika hiyo haki kamili. Yeye ajivunae kwa sababu ya neema, ajue hili na kufahamau ya kuwa wataoingia katika mlango huu wa neema ni wengi, lakini watakaokaa ndani ya ufalme wake ni hao wenye HAKI.


Lakini ni nani mwenye haki leo? Maana kanisa limeambiwa lote litubu, je, ni hao wasio kanisani ndio wenye haki? Naam, wao si wenye haki machoni pao, ni rahisi kuisikia sauti yake na kutii kama ilivyoandikwa;


31 Je! Katika hao wawili ni yupi aliyefanya mapenzi ya babaye? Wakamwambia, Ni yule wa pili. Basi Yesu akawaambia, Amin nawaambia, watoza ushuru na makahaba wanatangulia mbele yenu kuingia katika ufalme wa Mungu.

Mathayo 21


Maana walio wana wa ufalme ni vipofu, hawaoni, katika saa ya kuvaa magunia na kujipaka majivu, wamevaa mavazi ya sikukuu. 


ISIKILIZENI SAUTI YA BWANA!


Mawasiliano;

(+255) 0755 251 999.

MATENDO YA SHERIA NI NINI NA KWA NINI HAYALETI HAKI?

NEEMA, NA MAUTI ILETWAYO NA NEEMA!

ANDIKO HUUA BALI ROHO HUHUISHA

WASIO HAKI HUNENAJE KWA LUGHA?

HAKUTAKUWA NA UNYAKUO JUU YA KIZAZI HIKI!

        CHANGIA KUPITIA

 

          NMB:       22510119402

          MOBILE: 255755 251 999

​​

             MASHIBE ELIAS NTINGINYA

Wills:

+255 755 251 999

Mbezi, Dar es Salaam

  • Facebook
  • Instagram
  • X
  • TikTok
bottom of page