top of page

Mwanzo 2 (Biblia Takatifu)


¹⁶ Bwana Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema, Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula,
¹⁷ walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika.

Tumekwisha kujifunza katika masomo yaliyotangulia juu ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya, vile vile matunda ya mti huo. Hapa nataka tuangalie hasa ujuzi wa mema na mabaya ni nini?


Neno ujuzi linamaanisha maarifa, au ‘knowledge’ kwa lugha ya kiingereza. Lakini haiishii  hapo tu, bali ujuzi huu pia unatafsirika kama ubunifu au uumbaji au ufundi. Ni uwezo wa kutengeneza jambo fulani.


Upo ujuzi wa aina mbalimbali kama ujuzi wa ujenzi, ujuzi wa kusuka, ujuzi wa kuendesha vyombo vya moto, n.k. Lakini hapa tunatazama ujuzi mema na mabaya. Na ili tuujue inapasa kujua mema na mabaya ni nini! Mema na mabaya ni yale yaliyo mazuri au sawa kufanywa na yale yasiyo sawa kufanywa yaani yanachukiza au kukasirisha.


Lakini mema na mabaya yanategemea na roho ya yule atawalaye. Kwa mfano tunazo katiba kwa kila nchi ambazo zina muongozo wa mema na mabaya, yaliyo haki na yasiyo haki. Lakini katiba ya nchi hii hafanani na katiba ya nchi nyingine. Kosa moja katika katiba ya nchi hii linaweza lisiwe kosa katika nchi nyingine.


Pia mema na mabaya yanaweza kuwa hivi kulingana na katiba lakini yakawa kinyume kulingana na mtawala. Kama katiba inachukia ufisadi, na mtawala ni fisadi; ufisadi hautakuwa chukizo kwa mtawala. Na kwa sababu hiyo mema na mabaya yanaweza kubadilika kulingana na mtu, jamii na hata taifa.


Mema na mabaya kwa shetani ni tofauti na mema na mabaya kwa Mungu. Na kwa sababu hiyo tunapoangalia mema na mabaya kwamba kwa nini mema yawe hivi na mabaya yawe hivi ni kulingana na Mungu, lakini kwa upande wa watumishi wake walio na ujuzi wa mema na mabaya, tafsiri ya mema na mabaya itategemea na ujuzi wao bila kutegemea tafsiri ya Mungu.


Tutazame ujuzi wa nyoka,


1 Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya Bwana Mungu. Akamwambia mwanamke, Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile matunda ya miti yote ya bustani? 
2 Mwanamke akamwambia nyoka, Matunda ya miti ya bustanini twaweza kula; 
3 lakini matunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu amesema, Msiyale wala msiyaguse, msije mkafa. 
4 Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa, 
5 kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya. 
6 Mwanamke alipoona ya kuwa ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa, basi alitwaa katika matunda yake akala, akampa na mumewe, naye akala.
7 Wakafumbuliwa macho wote wawili wakajijua kuwa wa uchi, wakashona majani ya mtini, wakajifanyia nguo.

Mwanzo 3:1-7


Ujuzi wa nyoka ulikuja na tafsiri juu ya maneno ya Bwana aliyomwagiza Adamu, akisema hutakufa ukila matinda ya ujuzi wa mema na mabaya, bali utafanana na Mungu. tafsiri hii inapingana moja kwa moja na kile alichokisema Bwana Mungu juu tunda hilo. Bwana Mungu alisema wakila tunda watakufa (mwanzo 2:16-17), na nyoka anakataa kuwa sio kweli.


Maana yake nyoka ana ujuzi tayari wa kuamua mema ni yapi na mabaya ni yapi, hata kuweza kumpinga Mungu juu ya kifo. Ujuzi wake haukubaliani na wa Mungu na kwa sababu hiyo anawafundisha na wengine juu ya kile alichokisema Bwana kutumia ujuzi wao kufafanua maneno yake.


Lakini Nyoka alitoa wapi tafsiri hii? Maana alimhubiria Hawa kwa ujasiri na kumfanya aamini mpaka ilipokuwa dhahiri kwa Adamu na Hawa kuwa wamedanywa mara baada tu ya kula lile tunda. Roho wa Mungu akahuzunika ndani yao, wakajiona wa uchi.


Ujuzi wa mema na mabaya unatoka kwenye kujitegemea (self reliance), kuamua na kufanya pasipo kuhitaji usaidizi. Mtu akipata ujuzi huu kama alikuwa msaidizi wa fundi ujenzi, basi anaacha usaidizi na kuwa fundi ujenzi kamili. Maana yake kwa habari ya kufasiri neno la Mungu, mtu mwenye ujuzi wa mema na mabaya hategemei ufunuo wa Mungu kumpa kujua maana ya maneno aliyoyasema bali anaeweza kutumia ujuzi wake.



Na kwa sababu hiyo anakuwa hupo chini ya Mungu tena, kwa sababu ana uwezo wa kumwelewa bila kufundishwa na Yeye. Kwa maneno mengine anakuwa sawa na Mungu. Ndivyo shetani alivyo, ndivyo na nyoka alivyokuwa na watumishi wa uongo.


Mtu mwenye ujuzi wa mema na mabaya, anakuwa kama huyu nyoka, anatafsiri neno la Mungu kwa roho yake mwenyewe. Atahalalisha atakalolihalalisha, ataharamisha atakaloliharamisha. Hawezi kukosea kwa sababu yeye ni kama Mungu. 


Kumbuka Mungu ndiye aijuaye haki katika utimilifu wake, alikuwepo kabla ya mwanadamu na kabla ya kila kitu kuwepo. Yeye ndiye mwenye ujuzi wa mema na mabaya na mwalimu wa huo. Kwa sababu hiyo mwanadamu anapaswa kufundishwa na Mungu kupata ujuzi wa mema na mabaya kuanzia hatua ya kwanza hata utimilifu wake. 


Lakini kinyume chake mtu mwenye ujuzi wa mema na mabaya hategemei Mungu kuamua au kufanya mambo yake, anaweza kuhalalisha hili, akakemea lile, anaweza kutengeneza nabii, karama, uponyaji n.k, kwa sababu anao ujuzi. Yaliyo mema kwa Mungu yanaweza kuwa mabaya kwake, na yaliyo mabaya kwa Mungu yanaweza kuwa mema kwake.


Anaweza kmwita mtu nabii asiye nabii kwa Mungu, anaweza kumheshimu anayepaswa kudharauliwa kwa Mungu, anaweza kumweka hai anayepaswa kufa na kumuua anayepaswa kuwa hai, anaweza kumfanya huyu kuwa nabii wa mwisho asiye nabii wa mwisho wala kuwa nabii kwa Mungu.


Anaweza kumpa utuku asiye na utukufu uwao wote kwa Mungu, na kumnyima utukufu aliye na utukufu kwa Mungu. Anaweza kumfanya huyu kuwa mtakatifu na sio yule. Hakuna Mungu kwa mtu huyu watu hawa isipouwa yeye/wao wenyewe, wala Mungu hana nafasi ya kumrekebisha/kuwarekebisha kwa yeye/wao ni kama Mungu. Kazi yao/yake ni safi machoni pake yeye mwenyewe. Hizi ndio ibada za miungu.


Ujuzi wa mema na mabaya ndio unaotengeneza dini (ibada za sanamu) na pia ndio unaotengeneza madhehebu katikati ya ibada ya Mungu. Maana tafsiri za uongo (tafsiri zilitokana na ujuzi wa mema na mabaya) ndio neno la Mungu kwao watu hawa. Nazo zikiingia kwa watu wa Mungu wakazicha, kanisa zima humwasi Mungu.


Na baadae neno la Mungu huja kwao wapate kutubu, lakini kwa kujiona wako sawa na Mungu, hawana wa kumkosea wala kuwakosoa hawawezi kutubu. Ndipo Mungu huwaacha na ujuzi wao wa mema na mabaya kwa maana ya hiyo injili yao waliojitengenea kwa ujuzi wao. Nao huwa dhehebu, watu waliotapikwa au kukataliwa na Mungu! Na hapa ndipo inakuja tafsiri halisi ya ujuzi wa mema na mabaya kwa nini unaleta kifo, KWA SABABU HAWAWEZI TENA KUTUBU.


Kila aliye na ujuzi huu wa mema na mabaya, amekufa mbele za Mungu. Na hakuna dhehebu lisilo na ujuzi huu wa mema na mabaya. Maana kama nilivyotangulia kusema kizazi hiki kimekwisha kula tunda la ujuzi wa mema na mabaya. Na kwa sababu hiyo hakuna atakayeingia mbinguni kwa haki ya injili za madhehebu, isipokuwa neno la Mungu. 


Hii ndio sababu kwa nini Yesu Kristo alikwisha tamka hukumu kwa kizazi hiki cha kanisa kuwa atakitapika kama hawatatubu.


Ufunuo wa Yohana 3


¹⁴ Na kwa malaika wa kanisa lililoko Laodikia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye Amina, Shahidi aliye mwaminifu na wa kweli, mwanzo wa kuumba kwa Mungu.
¹⁵ Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto.
¹⁶ Basi, kwa sababu una UVUGUVUGU, wala hu baridi wala moto, NITAKUTAPIKA UTOKE KATIKA KINYWA CHANGU.

Laodikia ndio kizazi hiki cha kanisa, kilicho na ujuzi wa mema na mabaya, kimejaa mafundisho yaliyotokana na ujuzi wao wenyewe. Na kwa sababu ya ujuzi wao wamejitajirisha kwa ujuzi wao na machoni pao yaani Hekima zilizotokana na ujuzi wao wala hawana hatia. Ndipo utaona wanabishana na Mungu kuwa wao ni matajiri, si masikini wala vipofu wala uchi.


17 Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi.

Ufunuo wa Yohana 3


Lakini kanisa halijui hilo kwa sababu wamefasiri neno la Mungu kwa ujuzi wao wakajipa tafsiri zisizo Mungu na kunena yaliyo yatokanayo na wao wenyewe. Uvuguvugu huu maana yake ni mchanganyiko wa neno la Mungu na ujuzi wa mwanadamu wa mema na mabaya ndio theolojia.


Theolojia si neno la Mungu, ni ujuzi wa mema na mabaya wa mwanadamu juu ya neno la Mungu na kwa sababu hiyo anasema NITAKUTAPIKA, hakuna hata mmoja ataingia katika ufalme wake isipokuwa wametubu kwa KUITII SAUTI YAKE ibishao sasa mlangoni.


Ufunuo wa Yohana 3 (Biblia Takatifu)


²⁰ Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.


Mawasiliano;

+255 755 251 999


MATENDO YA SHERIA NI NINI NA KWA NINI HAYALETI HAKI?

NEEMA, NA MAUTI ILETWAYO NA NEEMA!

ANDIKO HUUA BALI ROHO HUHUISHA

WASIO HAKI HUNENAJE KWA LUGHA?

HAKUTAKUWA NA UNYAKUO JUU YA KIZAZI HIKI!

        CHANGIA KUPITIA

 

          NMB:       22510119402

          MOBILE: 255755 251 999

​​

             MASHIBE ELIAS NTINGINYA

Testaments :

+255 755 251 999

Mbezi, Dar es Salaam

  • Facebook
  • Instagram
  • X
  • TikTok
bottom of page