top of page

Baada ya Adamu na Hawa kula yale matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya, ile injili ya nyoka, walilaaniwa. Kwa lugha nyingine waliadhibiwa kwa makosa yao. 


9 Bwana Mungu akamwita Adamu, akamwambia, Uko wapi?
10 Akasema, Nalisikia sauti yako bustanini, nikaogopa kwa kuwa mimi ni uchi; nikajificha.
11 Akasema, Ni nani aliyekuambia ya kuwa u uchi? Je! Umekula wewe matunda ya mti niliyokuagiza usiyale? 
12 Adamu akasema, Huyo mwanamke uliyenipa awe pamoja nami ndiye aliyenipa matunda ya mti huo, nikala.
13 Bwana Mungu akamwambia mwanamke, Nini hili ulilolifanya? Mwanamke akasema, Nyoka alinidanganya, nikala.
14 Bwana Mungu akamwambia nyoka, Kwa sababu umeyafanya hayo, umelaaniwa wewe kuliko wanyama wote, na kuliko hayawani wote walioko mwituni; kwa tumbo utakwenda, na mavumbi utakula siku zote za maisha yako; 
15 NAMI NITAWEKA UADUI KATI YAKO NA HUYO MWANAMKE, NA KATI YA UZAO WAKO NA UZAO WAKE; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino.
16 Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa utungu utazaa watoto; na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala.
17 Akamwambia Adamu, Kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambao nalikuagiza, nikisema, Usiyale; ardhi imelaaniwa kwa ajili yako; kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako; 
18 michongoma na miiba itakuzalia, nawe utakula mboga za kondeni; 
19 kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi.

 

Mwanzo 3:9-19


Mstari wa 15 inatajwa adhabu ya uadui wa milele kati ya uzao wa nyoka na uzao wa mwanamke. Uzao wa nyoka unaozungumziwa hapa ni upi na uzao wa mwanamke ni upi?


Kwa miaka mingi imetafsirika kuwa uzao wa nyoka ni hao nyoka tunaowajua, wanaotambaa ardhini na uzao wa mwanamke ni wanadamu wote. Lakini hiyo sio kweli, kwa sababu si nyoka pekee aliye na uadui na mwanadamu bali simba, ng’e, chui, dubu, n.k, ni maadui pia.


Kila mnyama ana uadui na mwanadamu na kwa sababu hiyo tungepaswa kujua simba alifanya nini akalaaniwa kuwa na uadui na mwanadamu au ng’e au chui n.k. Ni kweli kwa dhambi ya nyoka laana ilienda kwa kila mnyama. Lakini nyoka ndiye aliyelaaniwa kuliko wanyama wenzake wote.


Lakini madhara yao yanafanana, sumu ya nyoka inaua, simba anaua pia, dubu n.k. Lakini kwa nini aseme uadui utakuwepo kati ya uzao wa nyoka na uzao wa mwanamke  wakati upo kwa wanyama wote?


UZAO WA NYOKA


Uzao wa nyoka aliokuwa anauzungumzia ni watu waliozaliwa na Hawa vile vile lakini kwa habari ya Mungu ni watu waliozaliwa kwa injili ya Nyoka. Ni watu waliozaliwa na mafundisho ya uongo kama ya nyoka. 


Uzao huu wakati mwingine huitwa uzao wa mwanadamu au uzao wa uongo. Nimekwisha kuelezea juu ya uzao huu wa nyoka katika somo hili;

https://www.injiliyayesujioni.org/sermons/uzao-wa-nyoka-ni-upi%3F


UZAO WA MWANAMKE


Uzao wa mwanamke ni uzao wa Mungu, watu waliozaliwa kwa Mungu kwa neno la Mungu litokalo katika kinywa chake. Hawa ndio huwasikiliza wanabii wa Mungu na kuingojea sauti yake wakati wa maovu.


UZAO WAKE UTAKUPONDA KICHWA NA WEWE UTAMPONDA KISIGINO.


15 nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino. 

Mwanzo 3:15


Injili ya nyoka haiji isipokuwa kuna neno la Mungu, maana injili ya nyoka ni ujuzi wa kufasri neno la Mungu kwa ujuzi wa kibinadamu. Hivyo wana wa Mungu kwa neno la Mungu huwapo kwanza kabla ya uzao qa nyoka.


Ndipo uongo hufuata ili kuliondoa neno la Mungu mioyoni mwa watu. Njia anayoitumia shetani kuteka watu waje kwenye uongo ni tofauti na njia anayoitumia Mungu kuwarudisha wale watu walioibiwa na shetani.


Wstumishi wa shetani kama alivyokuwa nyoka huja kwa watu wachanga kiroho, kama nyoka alivyomjia Hawa badala ya Adamu. Uongo wa shetani unaopingana na neno la Mungu huwavuta watu wachanga kiroho ambao wana injili ya maziwa na si chakula kigumu, hawajui neno la haki bado.


Shetani huwa haji kushindana na manabii wa Mungu anapoanza kushawishi watu waje kwake, hutumia waumini wasio na neno la haki bado kuwavuta kutoka kwenye kweli waje kwake.  Huko ndiko kuponda kisigino cha uzao wa mwanamke.


 Maana anavizia nyuma, na baada ya mda hujitwalia watumishi mbali mbali wanaotamani mkate na heshima (mathayo 4:4-7), na kuwagawia mali kama apendavyo ili kusimamisha ufalme wake mahali pa ufalme wa Mungu. Shetani huja kwa kujipendekeza akiwa na kitu mfukoni kama zawadi kwa yeye atakayemfuata.


Kisha baada ya mda shetani akiisha kufanikiwa katika uongo wake na kuligeuza kanisa limwelekee yeye. Bwana Mungu hutuma manabii wakiwa na ufunuo wa kuwepo kwa ule uongo. Hawa hawaji kama watumishi wa shetani wajavyo, manabii wa Mungu huja na neno kama nyundo juu ya vichwa vywa manabii wa ibilisi.


Neno lao huwa juu ya watumishi wa kanisa, wachungaji, walimu, wainjilisti, maaskofu, manabii n.k. Huko ndiko kuponda kichwa chwa nyoka. Kichwa cha nyoka ni watumishi wake, manabii wake, manabii wa uongo. Kila nabii aliuponda kichwa uzao wa nyoka Yeremia 23, ezekieli 13, Mathayo 3:7, Mathayo 23.


Neno lao ni juu ya kila neno lisilo Mungu ambalo limepandwa na watumishi hawa waliojiuza kwa shetani kwa ajili mkate na heshima ili waseme uongo juu ya Bwana.


ISIKILIZENI SAUTI YA BWANA.


Mawasiliano;


+255 755 251 999.

MANABII WA UONGO, Mahali wanakotoka

MANABII, NA AINA ZA MANABII

UJUZI WA MEMA NA MABAYA NI NINI NA KWA NINI NI DHAMBI

UADUI KATI YA UZAO WA MWANAMKE NA UZAO WA NYOKA

SABABU ILIYOPELEKEA ULIMWENGU WA KWANZA KUANGAMIZWA

        CHANGIA KUPITIA

 

          NMB:       22510119402

          MOBILE: 255755 251 999

​​

             MASHIBE ELIAS NTINGINYA

Testaments :

+255 755 251 999

Mbezi, Dar es Salaam

  • Facebook
  • Instagram
  • X
  • TikTok
bottom of page