top of page

Ufunuo wa Yohana 3


¹⁴ Na kwa malaika wa kanisa lililoko Laodikia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye Amina, Shahidi aliye mwaminifu na wa kweli, mwanzo wa kuumba kwa Mungu.
¹⁵ Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; INGEKUWA HERI KAMA UNGEKUWA BARIDI AU MOTO.
¹⁶ Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu.

Laodikia ndio kizazi hiki, ambacho ni vuguvugu, si moto wala si baridi. Lakini katika mstari wa 15,  Bwana anasema ingekuwa heri kwa Laodikia kama angekuwa baridi au moto kuliko kuwa vuguvugu.

Maana yake Laodikia amesimama mahali pa hasira ya Bwana, uvuguvugu ni chukizo kwa Mungu. 


Tena kwamba Laodikia ameihesabu kazi yake akaiona ni njema, akaridhiria ubatili na kufanya maridhiano na uongo. Ndipo Bwana anasema, ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto. Ni mambo mawili yaliyo heri kwa Laodikia, awe moto au awe baridi. Lakini Laodikia metoka katika ubaridi akaenda katika uvuguvugu, akaketi mahali hapo na kuridhika. Hana haja na kuwa moto.


KWA NINI NI HERI AGEKUWA BARIDI?


Kwa kuwa Laodikia ni kanisa, kuwa baridi kwa kanisa ni kuondoka kwa Mungu au kuachana na neno lake na kurudi katika ulimwengu kama hapo kwanza kabla ya kusikia neno la Mungu. Lakini Bwana Mungu anasema ni heri kanisa hili lingekuwa baridi kuliko kuwa vuguvugu.


Kanisa kuwa baridi maana yake si kanisa tena bali watu wa mataifa. Ni jukumu la Mungu kuwarehemu wenye dhambi yaani watu wa mataifa. Haji kwao kuwahukumu bali kuwaokoa, lakini ikiwa watu hao si watu wa mataifa bali watu walioitii sauti yake kisha baadae wasiifuate, ndipo huleta hasira.


Mtu mmoja katika shamba lake, alimtuma mojawapo ya wafanya kazi wake aende mjini akamchukukulie mahitaji yake, mfanyakazi wa kwanza akasema siwezi kwenda ni mbali. Wa pili akakubali kwa moyo mmoja, akaanza safari kuelekea mjini. Lakini alipokuwa nusu ya safari aliona watu wakiburudika kwa ngoma na matari. Moyo wake ukamshawishi akaribie katika sherehe hiyo.


Akazitumia pesa za bwana wake kwa anasa na vileo mahali pale, naye akajenga nyumba na kuishi hapo. Ni yupi kati ya mfanyakazi wa kwanza aliyekataa kwenda na yule wa pili aliyekubali kwenda lakini asirudi atakayemtia Bwana wake hasira iliyo kuu?


Naam, imeandikwa;


21 Utakapoweka nadhiri kwa Bwana, Mungu wako, usiwe mlegevu katika kuiondoa; kwa kuwa Bwana, Mungu wako, hataacha kuitaka kwako; nayo hivi itakuwa dhambi kwako.

Kumbukumbu la Torati 23


Naam, huyo wa pili alikubali kwenda ikawa nadhiri kwake, alitwaa mali za mwajiri wake hakuzirudisha wala kile alichotumwa,  na subira ya mwajiri ikageuka kuwa hasira kuu. Naye aliposikia aliyotenda yule mfanyakazi wake, akamwendea kwa jeshi kubwa ili kuharibu na kumwangamiza.


Lakini huyo wa kwanza hakumharibu wala kumwangamiza baada ya   kukataa, ijapokuwa hakumweka karibu naye. Ndivyo ilivyo kwa kanisa, ambalo limekubali kutii neno la Mungu lipate kuwa takatifu lakini likaishia njiani, likaanza kufuata yaliyo ya ulimwengu huu na desturi zake. Badala ya kutafta utakatifu, linatafta, gari, kujenga, kuona, kuolewa, pesa, biashara, baraka, nyota, kusafiri nje ya nchi, umaarufu, n.k.


Kwa sababu hiyo ni vuguvugu, ingekuwa heri lingekataa kutii au kurudisha kilicho cha Bwana na kusema siwezi kuendelea na safari hii. Maana yeye aliyewapa agano hilo anangoja wawe watakatifu kama Yeye alivyo mtakatifu. Lakini kanisa linatumia hilo neno lake kwa mambo yake na faida yake. LIMEMWACHA BWANA!


KWA NINI NI HERI KUWA MOTO?


Bwana Mungu amesema, ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto. Tumeona kuwa baridi ni nini, lakini kuwa moto ni kufikilia ukamilifu. Bwana Mungu anatazamia kuliona kanisa kama neno lake lilivyo. Yaani kulitimiza kusudi la neno lake, ni sawa na mafanyakazi aliyekubali kutumwa na mwajiri wake, akaenda mjini akachukua yale aliyoagizwa na kurudi.


Hivyo kanisa hili ambalo ni vuguvugu, linasubiri ghadhabu ya Bwana, watapokea mapigo zaidi ya hao waliokataa.


Imeandikwa;


47 Na mtumwa yule aliyejua mapenzi ya bwana wake, asijiweke tayari, wala kuyatenda mapenzi yake, atapigwa sana.
48 Na yule asiyejua, naye amefanya yastahiliyo mapigo, atapigwa kidogo. Na kila aliyepewa vingi, kwake huyo vitatakwa vingi; naye waliyemwekea amana vitu vingi, kwake huyo watataka na zaidi.

Luka 12:47-48.


Hivyo ghadhabu ya Bwana inafuka juu ya kanisa, si kwa hao waliokataa kutii neno lake. Ijapokuwa pia wote watahukumiwa.


ISIKILIZENI SAUTI YA BWANA!


Mawasiliano:

+255755251999

MANABII WA UONGO, Mahali wanakotoka

MANABII, NA AINA ZA MANABII

UJUZI WA MEMA NA MABAYA NI NINI NA KWA NINI NI DHAMBI

UADUI KATI YA UZAO WA MWANAMKE NA UZAO WA NYOKA

SABABU ILIYOPELEKEA ULIMWENGU WA KWANZA KUANGAMIZWA

        CHANGIA KUPITIA

 

          NMB:       22510119402

          MOBILE: 255755 251 999

​​

             MASHIBE ELIAS NTINGINYA

Testaments :

+255 755 251 999

Mbezi, Dar es Salaam

  • Facebook
  • Instagram
  • X
  • TikTok
bottom of page